Tuesday, November 11, 2014

POLISI YAWATAWANYA WAFUASI WA MBOWE KWA MABOMU


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Freeman Mbowe 

Wafuasi wa (Chadema) wilayani Mpanda jana jioni walilazimika kutafuta vichochoro vya kukimbilia baada ya polisi kusambaratisha kwa mabomu ya machozi, maandamano ya kumsindikiza Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe baada ya mkutano.

Patashika hiyo ilitokea baada ya mkutano wa Mbowe kumalizika na wafuasi wake kutaka kumsindikiza hotelini, jambo ambalo polisi hawakulikubali.

Baada ya wananchi hao kuanza maandamano hayo, polisi walifyatua mabomu takriban 15 yaliyowafanya wafuasi wote kutawanyika na kusababisha taharuki miongoni mwa wakazi wa mji huo. Dakika chache baada ya tukio hilo, umeme ulikatika mji mzima.

Tofauti na maeneo mengine aliyofanya ziara zake kama Tabora, Sikonge na Igunga ambayo wafuasi walikuwa wakimsindikiza, polisi wa Mpanda walijipanga ipasavyo tangu mapema kuhakikisha hali hiyo haitokei. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

INTERPOL YAWASAKA WACHINA 30 KWA UJANGILI WA TEMBO

Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav Babile 

Siku tano baada ya Serikali kukanusha vikali ripoti ya Shirika la Kimataifa la Mazingira (EIA) iliyoihusisha China na utoroshaji wa meno ya tembo nchini wakati wa ziara ya Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping mwaka jana, Shirika la Polisi la Kimataifa (Intepol), Tawi la Tanzania limesema linawatafuta raia zaidi ya 30 wa China ambao wanatuhumiwa kusafirisha meno ya tembo na kufanya uharamia wa kimazingira katika hifadhi za Taifa nchini.
Kauli ya Interpol inakuja huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu kashfa hiyo iliyosambaa wiki iliyopita kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa ambayo hata hivyo, Serikali imekanusha kupitia Ikulu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maliasili na Utalii huku ubalozi wa China nchini nao ukitoa tamko la kukanusha taarifa hizo.
Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav Babile alisema jana kuwa raia hao wa China wanatafutwa popote walipo duniani na hivyo watakapopatikana watakamatwa.
“Tunawatafuta popote duniani kwa usafirishaji wa meno ya tembo na uharamia wa mazingira, wakipatikana watachukuliwa hatua,” alisema Kamishna Babile. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ASKOFU ANASWA NA UNGA!

          
KIMENUKA! Vigogo wa madawa ya kulevya wakiwemo viongozi wa dini sasa wanaanza kupukutika kutoka kwenye mstari wa siri huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi kufuatia oparesheni kali inayofanywa na Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulenya Tanzania kuwanasa kila kukicha, Uwazi  lina mchoro kamili.Askofu Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Hivi karibuni kikosi hicho kimemkamata askofu (mwangalizi mkuu wa kanisa) aliyetambulika kwa jina la Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria ambaye ana kanisa la kiroho maeneo ya Sinza jijini Dar.
Jina la kanisa hilo limedhibitiwa na vyombo husika kwa sababu ya uchunguzi zaidi na uhalali wake wa kuwepo nchini.
SIKU YA TUKIO
Vyanzo vyetu makini ndani ya kikosi kazi vinaeleza kwamba, mchungaji huyo alikamatwa Oktoba 31, mwaka huu saa kumi usiku Tegeta wilayani Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroine kilo 35.
KAMA UNGEINGIA SOKONI
 Habari za ndani kutoka kwenye oparesheni hiyo zinasema kuwa, endapo unga huo ungeingia sokoni na kununuliwa, basi mtumishi huyo wa Mungu angevuna kitita cha zaidi ya shilingi bilioni mbili.
NYUMBA ALIYONASIWA YA PROFESA
Mchungaji huyo ambaye serikali imeanza kazi ya kulichunguza kanisa lake, alidakwa na mzigo huo haramu kwenye makazi aliyopanga ambayo ni nyumba ya profesa mmoja wa chuo kikuu, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Askofu akiwa chini ya ulinzi.
WASHIRIKA NAO WADAKWA
Kwa mujibu wa chanzo, kamatakamata ya mchungaji huyo pia iliwakumba watuhumiwa wengine ambao ni Walyat Khan raia wa Pakistani, Chuksi Sylvester Agbazuo na Tony Olafor wote raia wa Nigeria na inadaiwa kwamba walikuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali na kutoroka.
HABARI NYETI
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MKE ANAYEISHI NA WAUME WAWILI MAPYA YAIBUKA


Sakata la mke kuishi na waume wawili  limechukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa mume halali, Rogers Halinga kuketi kikao katika Kijiji cha Ishungu, Kata ya Ruiwa Mbarali, mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni mahakamani na kudai fidia.
Rogers Halinga akiwa na baba yake mzee Jason Halinga na mtoto anayedaiwa kugombaniwa.
Kikao hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa baba mzazi wa Rogers, mzee Jason Halinga (95), Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki nia ilikuwa kumsikiza mke wa Rogers, Juliana (22)  ili abainishe ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya mumewe (Rogers) na Biton Mwashilindi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ROONEY AKIJIANDAA KUICHEZEA ENGLAND MCHEZO WA 100,ATEMBELEA SHULE YAKE YA MSINGI

7
Mshambuliaji wa England Wayne Rooney akijiandaa kuandika historia ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioichezea timu yao ya Taifa michezo 100 na zaidi.
Mara nyingi wachezaji wa England wanapokuwa wamecheza michezo 99 huwa na utamaduni wa kwenda kwenye shule zao na kupigia picha na jumla ya wanafunzi 99
England inajiandaa kucheza mchezo wa kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Slovenia mwishoni mwa juma hili kwenye dimba la Wembley,huenda Rooney ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho akatimiza mchezo wa 100 siku iyo na kuwa mchezaji wa 9 kuichezea England michezo 100.
6 Baadhi ya wachezaji wengine waliofanikiwa kuvaa jezi ya England mara 100 na zaidi katika kipindi cha miaka 142 tangu timu hiyo ianzishwe ni: 5 Peter Shilton, David Beckham, Steven Gerrard, Bobby Moore, Ashley Cole, Frank Lampard, Bobby Charlton na Billy Wright – Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MADEREVA WA KAMPUNI YA MWANANCHI (MCL) WAKAMATWA NA MIRUNGI

  Polisi mkoani Iringa wanawashikilia watu watatu wakiwamo madereva wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11 alfajiri katika kituo cha ukaguzi cha Igumbilo mkoani hapa nabaada ya ukaguzi polisi walibaini magunia mawili ya mirungi ndani ya gari la kusafirishia magazeti ya kampuni hiyo.
Mungi alisema mirungi hiyo ilipakiwakatika eneo la Chalinze mkoani Pwani na taarifa za awali zinaeleza kuwa ilikuwa ikisafirishwa kwenda Zambia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 11, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI 47 WAUAWA SHULENI

Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakishambulia eneo hilo la Potiskum

Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Duru zinasema kuwa wanafunzi 47 wameuawa katika shambulizi hilo linalosemeklana kufanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa amevalia sare za shule.
Shambulizi lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule hiyo ni ya mafunzo ya sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa alisikia mlio mkubwa wa kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

USALAMA MDOGO, BENI DRC

Kikosi cha UN, DRC kinashutumiwa kwa kutolinda usalama vya kutosha
Baada ya miezi kadhaa ya utulivu katika eneo la mashariki mwa DRC, ghasia zimerejea tena.
Zaidi ya watu 120 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa kwa mapanga na mashoka mwezi uliopita katika eneo la mpakani na Uganda.
Inadhaniwa kuwa kundi la waasi kutoka nchini Uganda la ADF ndilo linalohusika na mashambulizi hayo.
Vikosi cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MONUSCO kimekuwa kikilalamikiwa katika mji huo wa Beni kwa kushindwa kuzuia mauaji, licha mamia ya wanajeshi wake kuweka kambi katika eneo hilo.
Lakini hata hivyo wenyewe wanasema ni vigumu kuweza wakuwalinda raia wote, licha ya kuchukua hatua kadhaa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SOCIEDAD WAMUITA MOYES KUWA MENEJA

David Noyes
Kocha wa zamani wa timu ya Manchester United David Moyes ametajwa kuwa meneja mpya wa timu ya kutoka Hispania,Real Sociedad.
Kocha huyo mwenye miaka 51, hii ni kazi yake ya kwanza baada ya kutimuliwa kwenye kilabu cha Man U mwezi wa nne mwaka huu, .
Moyes anachukua nafasi ya Jagoba Arrasate ambaye pia ametimuliwa na Sociedad baada ya matokeo mabaya na kusababisha timu hiyo kuangukia nafasi ya 15 katika ligi kuu nchini humo, maarufu kama La Liga.
Mkataba wa Moyes na Real Sociedad ni mpaka june mwaka 2016 na kwama mara ya kwanza ataonekana katika mechi ya Deportivo November 22. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NANI MWENYEJI WA CAF 2015...???



Kombe la mataifa ya Africa

Hatma ya nani atakuwa mwenyeji wa kombe la mataifa ya Africa 2015 maarufu kama Africa Cup of Nations lazima ajulikane, kwani kamati ya shirikisho la vilabu vya soka barani Africa imekutana kujadili juu ya suala hili .
Morocco ndiye aliyekuwa anapewa nafasi kubwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kuanzia tarehe 17 mwezi wa kwanza hadi mwezi wa pili tarehe 8, lakini kuna kila dalili Morocco inataka kuahirisha michuano hiyo kwa hofu dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola kuwa utaingia nchini humo.
Leo ndiyo leo, leo inapaswa kuwa siku ya kuamua kati ya Morocco na bodi ya shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF, ile sintofahamu baina yao inatatuliwa.
Mwishoni mwa wiki iliyopita waziri wa michezo wa Morocco,alisimama na kuongea kwa kifupi yakwamba hawataweza kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na badala yake wasikilizwe ombi lao la kuahirishwa kwa michuano hiyo mpaka mwaka wa 2016.
Wakati hayo yakijiri CAF wametoa msimamo wao ya kuwa tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo haitabadilika,sasa swali linakuja je CAF wana nchi nyingine iliyotayari kupokea michuano hiyo na kuwa mwenyeji? Ilhali imebakia wiki kumi tu? Na kama inawezekana basi itakuwa ni kati ya nchi zilizokuwa wenyeji wa michuano hiyo miaka ya karibuni,ambayo CAF ina uhakika na miundo mbinu yake na uwanja ulio tayari ndani yake.
Mnamo mwaka 2013, mwenyeji wa michuano hiyo ilikuwa ni Africa Kusini ambayo tayari imekwishatoa msimamo wake kuwa wala wasiitie mawazoni kuwa wao ndo kimbilio la kunusuru michuano ya mwaka huu.
Nao CAF sasa wanatarajiwa kutoa tamko lao la mwisho juu ya suala hili, haraka iwezekanavyo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, November 10, 2014

UTATA TENA: MISS TANZANIA MPYA SI RAIA WA TANZANIA...??!

Baada ya taji la Miss Tanzania kuvishwa kwa mshindi wa pili, utata mwingine umeibuka baada ya mrithi huyo, Lilian Kamazima kudaiwa kuwa si raia.

Jana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa Lilian siyo raia wa Tanzania na kwamba anatokea Rwanda.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim ‘Uncle’ Lundenga alisema tuhuma hizo kuhusu Lilian siyo kweli. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE 'AMWAGA SUMU' NYUMBANI KWA SAMUEL SITTA...!!!


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Extended mjini Urambo, Tabora alikohutubia mkutano wa hadhara juzi. 


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.

Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.

Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

IKULU: "TUMEFEDHEHESHWA KWA KITENDO CHA JAJI WARIOBA KUSHAMBLIWA"


Balozi Ombeni Sefue


Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.

Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.

“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.

“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”

Kauli hiyo ya Sefue imekuja wakati mdahalo huo uliovunjika baada ya Mzee Warioba kushambuliwa, ukiwa umetangazwa kufanyika upya Jumapili Novemba 16, mwaka huu katika hoteli hiyohiyo.

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole alithibitisha jana kuandaliwa kwa mdahalo huo kuanzia saa 9.00 alasiri siku hiyo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 10, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...