Katuni inayoonyesha ujambazi wa kutumia pikipiki na bastola unavyoshika kasi jijini Dar es Salaam.
Ni roho mkononi. Hayo ndiyo
maneno matatu yanayofaa kuelezea hali ilivyo jijini Dar es Salaam na
maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa pale mtu anapobeba fedha nyingi.
Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa
sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa,
kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.
Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupata taarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.
Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum
Mashati alisema: “Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka
benki. Eti majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa
una kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”
Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo
Mlimani City, ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai
hayo... “Si kweli kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya
uhalifu huu. Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu
wanapohudumia wateja.
“Hata mteja anapoingia benki hukatazwa kuongea na
simu au kuandika ujumbe. Mazingira tuliyojiwekea hayaruhusu kabisa
mawasiliano kati ya benki yetu na watu wa nje wakati wa kazi. Nadhani
vitendo hivi vya ujambazi vinaanzia kwa wateja wenyewe kutoa taarifa juu
ya mipango yao kwa watu ambao si waaminifu,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz