Wednesday, August 27, 2014

URAIS 2015 WAIBOMOA BONGO MUVI




KUMEKUCHA! Baada ya kuwepo kwa misuguano ya chini kwa chini kati ya viongozi na wanachama wa kundi la waigizaji wa filamu la Bongo Movie Unity, sasa siri imefichuka kuwa baadhi ya watu wanaotajwa kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wagombee urais mwakani, ndiyo wanaolibomoa kundi hilo kutokana na fedha wanazodaiwa kuzitoa.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Baadhi ya waigizaji wenye ushawishi katika kundi hilo waliliambia gazeti hili juzi kwamba, dhambi kubwa inayolitafuna kundi hilo ni kambi za kisiasa zinazoratibiwa na makada wawili wanaoonekana kuwa na ushawishi ndani ya CCM ambao wanatajwa kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete.


“Unajua hapa Bongo Muvi kuna watu wamejikita moja kwa moja katika hizi kambi ambazo kuna waheshimiwa hawa wawili (majina tunayo) ndiyo sababu kuu ya watu wengine kufikia kujiuzulu kwa hoja kuwa wanatumika kwa manufaa ya mtu,” alisema mmoja wao aliyeomba hifadhi ya jina lake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Inadaiwa kuwa waheshimiwa hao wawili wamekuwa wakitoa fedha ili kufadhili hafla mbalimbali zinazowahusu waigizaji hao kwa lengo la kutaka kuwatumia muda rasmi wa kampeni utakapowadia.
“Hata hizi hafla zinabuniwa na kuratibiwa na wakubwa hao ambao hutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kuzifanikisha. Mfano, kujiuzulu kwa Katibu wa Bongo Muvi, Mtitu (William) kulitokana na kuyeyuka kwa fungu lililotoka kwa… (anataja jina).
“Sasa Mtitu akaona huu ubabaishaji, watu wengine wanufaike wao watumike tu,” alisema mtoa habari huyo.Akizungumzia hitima ya kuwaombea wasanii wa filamu waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambako Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa (CCM) Abdallah Bulembo alikuwa mgeni rasmi, mtoa habari hii alisema kuna ‘fungu’ lilitoka.
Katibu wa Bongo Muvi aliyejiuzulu,  Mtitu aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanatumika kisiasa kwa faida ya watu wengine.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu.
“Nimechoka kutumiwa kisiasa bila ridhaa yangu, kisingizio Bongo Muvi, kama kuna mtu au chama kinataka kututumia wasanii au kuitumia Bongo Muvi basi kuwe na uwazi na siyo kumtumia mtu mmoja kwa manufaa yake mwenyewe,” alisema.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alikiri kuzisikia siku nyingi, tokea alipoandaa chakula cha usiku kwa wadau wake katika Hoteli ya Great Wall iliyopo Masaki jijini Dar.
“Unajua si kila kitu ni siasa na yote haya yanasemwa kwa kuwa mimi niko kambi ya huyo mheshimiwa. Kwa vile likitokea jambo lolote Bongo Muvi mi huwa naenda kwake kuomba msaada.
“Halafu hakuna mwana Bongo Muvi asiyejua kuwa akaunti yetu ipo tupu, sasa nikienda kuomba fedha naambiwa niko kambi yake, hilo halina ukweli wowote,” alisema Steve anayehisiwa kuwa kambi hiyo.
Akikanusha madai ya kutafuna shilingi milioni 22 kati ya hizo, saba zikiwa ni malipo waliyochukua kwa ushiriki wao katika tamasha moja na zilizobaki zikiwa ni michango kutoka kwa matajiri mbalimbali, Steve alisema:
“Ilitoka shilingi milioni saba kwa ajili ya tamasha, huyo Mtitu ni mmoja wa watu waliokula zile fedha lakini hazungumzi chochote.
Kuhusu kupewa milioni kumi na tano na huyo mheshimiwa ili nifanye dua pale Karimjee Hall si kweli, kuna watu kibao wametoa misaada yao na uzuri zaidi hakuna aliyetoa fedha taslimu zaidi ya kusema mimi nitafanya kitu fulani na wamefanya, mimi namsihi Mtitu awe mkweli tu katika hili asituchonganishe.”
Makada wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho 2015 ni Edward Ngoyai Lowassa, Frederick Tuluway Sumaye, Steven Masatu Wassira, January Yusuf Makamba, Bernard Camillius  Membe, Wiliam Mganga Ngeleja, Samuel John Sitta na hivi karibuni Mizengo Peter Pinda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Chanzo GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...