Wednesday, August 27, 2014

DI MARIA ASAINI MIAKA 5 MAN U

WINGA Angel di Maria amejiunga rasmi na klabu ya Manchester United kwa ada ya pauni milioni 59.7 kwa mkataba wa miaka mitano.

Angel di Maria akipozi na Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal.
Di Maria amekamilisha usajili huo leo usiku na atakuwa akilipwa pauni 200,000 kwa wiki nyuma ya Wayne Rooney anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Staa huyo aliyetokea Real Madrid amevunja rekodi ya Ligi Kuu ya England kwa uhamisho wake wa bei ghali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Di Maria akiwa na jezi ya Man U.
Baada ya kukamilisha usajili huo, Di Maria alisema : 'Manchester United ndiyo klabu pekee ambayo ingeweza kunifanya niondoke Real Madrid'
Di Maria anaungana na wachezaji wengine wapya klabuni hapo kama Marcos Rojo, Ander Herrera na Luke Shaw.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...