Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za
hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi
25, mwaka huu, walinaswa na kamera za Global kwenye hoteli moja yenye
hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
The Biggest
IQ, Ijumaa Wikienda, linathubutu kwa kuwa lina ushahidi wa kutosha
kutamka kwamba Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba
namba 208, waliingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na
saa 9:13 mchana.
Monday, April 08, 2013
Tigo yawekeza kuunganisha watu wa vijijini na kuboresha huduma zake.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akihutubia wananchi wa wilaya
ya Kasulu kwenye sherehe za uzinduzi wa minara. Kulia kwake Meneja wa
Kanda ya ziwa Bw Joseph Mutalemwa na Meneja wa Tigo wa mkoa wa Kigoma
Bw Gamu Kimoro.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akitaka utepe kuzindua mnara
ya TIGO katika kata ya Muyama wilayani Buhigwe. Kulia kwake Meneja wa
kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.
Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke nchini Uingereza Baroness Thatcher afariki dunia.
Waziri
mkuu wa zamani nchini Uingereza Bibi Margret Thatcher amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Thatcher
aliyekuwa mwanake wa kwanza kushika wadhfa huo, alikuwa alitokea chama
cha Conservative na kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 1990.
Waziri
Mkuu wa sasa nchini humo Bw. David Cameron ameelezea masikitiko yake na
kumuita mwana mama huyo kuwa mjasiri wa Uingereza.
Naye
Malkia Elizabeth wa II wa nchi hiyo hakusita kueleza kushitushwa na
habari za kifo hicho huku akisema kimemhuzunisha lakini heshima ya
kiongozi huyo itabaki palepale.
Kwa
mujibu wa taarifa kiongozi huyo hatazikwa kwa mazishi ya kitaifa lakini
atazikwa kwa hadhi sawa na Princes Diana nay a Mama wa Malkia.
Waziri
Mkuu wa Uingereza Bw. Cameron ambaye yuko ziarani nchini Hispania kwa
ajili ya mikutano, amelazimika kukatisha ratiba ya mazungumzo yake na
rais wa Ufaransa Francois Hollande na kurejea nyumbani.
Lady
Thatcher kama alivyokuwa akijulikana alizaliwa akiitwa Margaret Roberts
na kuhudumu kama mbunge wa Finchley –London Kaskazini tangu mwaka 1959
hadi 1992.
ANGALIA TUKIO LA WACHAWI WAWILI WALIODONDOKA NA UNGO HUKO KAHAMA- SHINYANGA...
WAZEE
WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA
POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI
(80)
Watu
wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha
Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika
mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.
Watu
hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na
Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo
wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa
shughuli za kishirikina.
Katika maelezo yao wazee hao wamedai kuwa
wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo
waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa
wanaelekea.
Chadema kuwasha moto bungeni, ni kuhusu wanachodai 'utendaji usiofaa' wa Bunge.
Wakati
Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho, Kamati Kuu ya
Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulibana Bunge
kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na Spika na
wasaidizi wake.
Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8, mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.
Kambi
ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa kwa hoja binafsi za baadhi
ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Maji), James
Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari, ambaye hoja yake ilihusu
utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.
Jana,
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Kamati
Kuu ilibaini kwamba matukio yaliyotokea katika kikao 10 yalitokana na
meza ya spika kutofuata kanuni.
MKAPA AWATAKA VIONGOZI WAFUATE MISINGI YA NYERERE
Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila
ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria
kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Akitoa
salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la
Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na
waumini wa
madhehebu yote.
Sunday, April 07, 2013
LULU AONGOZA WASANII NA WENZIE KUTEMBELEA KABURI LA KANUMBA NA KUKUTANA NA MAMA KANUMBA.
Lulu akiwa na mama yake mzazi leo walipo tembelea kaburi la marehemu Steven Kanumba ikiwa ni mwaka mmoja toka amefariki |
Wakimuombea Marehemu Steven Kanumba |
ANGALIA PICHA ZA BONGO MOVIES WAKIPATA LUNCH NYUMBANI KWA WEMA SEPETU
CEO wa kampuni ya Endless Fame Pro' Wema Sepetu Leo amewaalika wasanii wenzake wa Bongo Movie Nyumbani kwake Kijitonyama kujumuika nae kwa pamoja kwenye Chakula cha mchana..... |
Hatman & Irene Uwoya |
ANGALIA PICHA ZA NDOA YA MZEE PHILIP MANGULA NA MWALIMU YOLANDA KABEREGE, JANA
Akifungisha
Ndoa Hiyo Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya
Mengele Amekumbusha Maneno ya Mungu na Kuwataka Wanandoa Kuishi Kwa
Misingi ya Dini Kama Ilivyoelekezwa Kwenye Vitabu Vya Dini.
Kulia ni mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwa na waziri mkuu Mizengo pinda katikati akifuatiwa na Katibu mkuu wa CCM.
Kushoto
ni msemaji wa familia ya mzee Philip Mangula Dr.Lechion Kimilike
ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu huria cha Tanzania Tawi la
Njombe[NJOMBE OPEN UNIVERSITY].
Saturday, April 06, 2013
MSANII WA BONGO FLEVA AFARIKI DUNIA KWA KUJIDUNGA SINDANO ZA MADAWA YA KULEVYA....!!
MSANII
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya aliyetambulika kwa jina moja la
Rocky mkazi wa Kawe, Dar amefariki dunia baada ya kujidunga madawa ya
kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo na kuomba hifadhi ya jina lake, marehemu anayekadiriwa kuwa na umri wa
Ray C
AFUNGWA MIAKA 10 JELA KWA KOSA LA "KUMPIGA DENDA" NA KUMTOMASA UKENI BINTI WA MIAKA 13 HUKO MPANDA
MAHAKAMA
Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41)
mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela
kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13,
anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa
yake.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo
jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali
katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo
aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi
30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.
Ilidaiwa
kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni akielekea
nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya nyumba yake
ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa nguvu nyumbani
kwake.
MAHAKAMA
Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41)
mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela
kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13,
anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa
yake.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo
jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali
katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo
aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi
30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.
Ilidaiwa
kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni akielekea
nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya nyumba yake
ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa nguvu nyumbani
kwake.
Subscribe to:
Posts (Atom)