Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akihutubia wananchi wa wilaya
ya Kasulu kwenye sherehe za uzinduzi wa minara. Kulia kwake Meneja wa
Kanda ya ziwa Bw Joseph Mutalemwa na Meneja wa Tigo wa mkoa wa Kigoma
Bw Gamu Kimoro.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akitaka utepe kuzindua mnara
ya TIGO katika kata ya Muyama wilayani Buhigwe. Kulia kwake Meneja wa
kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.
Mkuu
wa wilaya Buhigwe Mh Charles Bishuli akikabidhi vitabu 1,000 vya
sayansi kutoka kampuni ya simu za mkononi TIGO, kwa mwalimu mkuu wa
shule ya msingi Nyaminkunga Bw Hamisi Bunoge.
Tigo
Tanzania leo wametangaza mipango yao ya kuwekeza katika upanuzi wa
mtandao wake ili kuongeza kiwango cha ubora na upatikanaji wa mtandao
huo nchini kote. Upanuzi huo pia utakwenda sambamba na kujenga
miundombinu mipya ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini, kuleta
mawasiliano kwa maelfu ya watu. Minara mipya ya mawasiliano itajengwa
nchi nzima ambapo mradi huo utaanzia katika maeneo kama Mwanza, Tabora,
Kigoma, Mara na Kagera.
Kwa
kuanzia mkoa wa Kigoma Tigo imeboresha mtandao kwaku zindua minara
mitatu (3) katika Tarafa ya Mwandiga wilaya ya Kigoma vijijini,Kata ya
Muyama wiliaya mpya ya Buhigwe na Kazuramimba wilaya ya Uvinza.
Akizindua
Minara hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Issa Mashibya ,Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mh.Charles Gishuli alisema Uzinduzi wa minara hii
mipya wa mawasiliano hapa leo hii itatuwezesha kutumia mtandao wa Tigo
kwa kutoa mawasiliano yenye ubora wa hali ya juu hivyo kufurahia zaidi
mawasiliano ya simu zetu za mkononi. Matumaini na imani yangu kuwa, hii
ni mojawapo ya mambo mengi mazuri kutoka Tigo na ninatarajia mambo
mengine makubwa na mazuri zaidi kuja kupitia mtandao huu kwa siku
zijazo.
Akitangaza
mradi huo, kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Meneja wa Kanda
ya Ziwa Bw. Joseph Mutalemwa alisema “Tigo Tanzania imeendelea kukua kwa
kasi mwaka hadi mwaka. Bidhaa zetu za kipekee na huduma pamoja na
kuongezeka kwa wateja ni ushahidi wa wazi kabisa wa kukua kwetu.
Uzinduzi wa minara hii mipya utawezesha kuwapatia wateja wetu bidhaa
bora za kipekee zilizobuniwa katika ubora wa hali ya juu ili wateja wetu
waweze kunufaika na huduma na bidhaa zenye kiwango cha hali ya juu
kabisa kwa hatua mpya. Hii ndio dhamira yetu ambayo imetufanya tuendelee
kuwa kampuni inayoongoza ya mtandao wa simu za mkononi Tanzania.”
Kwa
kanda ya Ziwa Tigo ina mpango wa kuboresha minara 141 hadi kufikia mwezi
septemba ambapo tayari minara 17 imeshawaka, kati ya hii 17, mitatu
(3) ndiyo iliyozinduliwa Kigoma na lengo kubwa nikuwasha minara 24 kwa
mkoa wa Kigoma.
Tukiwa
tayari na mtandao imara wa mawasiliano katika mikoa mingi ya Tanzania
bara na Zanzibar, upanuzi huu wa mtandao wetu unalenga kuhakikisha kuwa
mtandao wetu unapatikana katika mikoa mingi zaidi nchini. Itaboresha
ubora wa mtandao katika maeneo ambayo tayari yana mtandao wa Tigo
kuhakikisha mawasiliano yanaboreka zaidi na huduma za Intaneti
zinapatikana vizuri zaidi na wakati huo huo kuhakikisha kuwa tunapeleka
huduma za mtandao wa Tigo nje kidogo ya Tanzania, kuwawezesha wateja
wapya kuungana na wenzao ulimwenguni na kuwa sehemu ya jamii kubwa ya
mtandao wa mawasiliano ya simu.
“Tukiwa
tunajiamini katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano ya simu na nia
ya kuendelea kusonga mbele zaidi kwa siku zijazo, tumeona umuhimu wa
kupanua na kuboresha mtandao wetu. Uzinduzi wa minara hii mipya
utatuwezesha kupanua huduma zetu za mawasiliano katika maeneo haya
mapya, kwa wateja tulionao na tutakaokuwa nao kama tunavyodhamiria”
Pia
katika kufanikisha uzinduzi huo kampuni ya Tigo ilitoa vitabu 1000 vya
sayansi katika shule ya msingi ya Nyaminkunga Tarafa ya Muyama Wilaya
ya Buhigwe kama sehemu ya mchango wao kwenye sekta ya elimu, akipokea
vitabu hivyo mwalimu mkuu wa shule hiyo bw.Hamisi Bunoge ameishukuru
sana kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa mchango huo kwa kutambua
umuhimu wa elimu katika nchi yetu ya Tanzania
Katika
ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya
robo mwaka ya mawasiliano ya mwezi Septemba 2012, idadi ya wateja wa
Tigo iliongezeka kwa 20% kati ya mwezi Juni mwishoni 2012 na Septemba
30, 2012 ikiwa na wateja 630,000 walioripotiwa. Tukiwa na mikakati hii
ya upanuzi, tunatarajia kukua zaidi kwa mwaka huu 2013.
“SMILE, YOU ARE WITH TIGO”.
No comments:
Post a Comment