Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila
ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria
kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Akitoa
salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la
Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na
waumini wa
“Katika
kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa
wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za
kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote
kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika
jamii,” alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka
1995-2005.
Mkapa
alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.
“Wakati
wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia
wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,”
alisema.
Mkapa
ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa
lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha
uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.
Pia
alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na
kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.
Mkapa
alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya
kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na
Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao
katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya
Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake
haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.
Katika
hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na
kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na
yale ya Kiislamu.
Maneno
ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa
limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio
makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na
Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.
Pia
kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa
Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na
Tunduma.
Askofu
Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa
amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye jana alitaja vyanzo vya
vurugu zinazoendelea nchini kuwa unatokana na tofauti kubwa kati ya
walionacho na wasionacho.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua santuri ya nyimbo za dini kwa Kwaya ya Mt Joseph, Mfanyakazi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Sumaye
alionya kuwa kama hali ya utajiri kwa baadhi ya watu itaachwa na
kuendelea hivyo, ni wazi kuwa nchi haitatawalika kwa amani.
“Binadamu mwenye njaa na aliyekata tamaa kamwe hawezi kutawalika kwani kila wakati anahisi kutengwa na kundi jingine,” alisisitiza Sumaye.
SOURCE::MWANANCHI::
No comments:
Post a Comment