Waziri
mkuu wa zamani nchini Uingereza Bibi Margret Thatcher amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Thatcher
aliyekuwa mwanake wa kwanza kushika wadhfa huo, alikuwa alitokea chama
cha Conservative na kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 1990.
Waziri
Mkuu wa sasa nchini humo Bw. David Cameron ameelezea masikitiko yake na
kumuita mwana mama huyo kuwa mjasiri wa Uingereza.
Naye
Malkia Elizabeth wa II wa nchi hiyo hakusita kueleza kushitushwa na
habari za kifo hicho huku akisema kimemhuzunisha lakini heshima ya
kiongozi huyo itabaki palepale.
Kwa
mujibu wa taarifa kiongozi huyo hatazikwa kwa mazishi ya kitaifa lakini
atazikwa kwa hadhi sawa na Princes Diana nay a Mama wa Malkia.
Waziri
Mkuu wa Uingereza Bw. Cameron ambaye yuko ziarani nchini Hispania kwa
ajili ya mikutano, amelazimika kukatisha ratiba ya mazungumzo yake na
rais wa Ufaransa Francois Hollande na kurejea nyumbani.
Lady
Thatcher kama alivyokuwa akijulikana alizaliwa akiitwa Margaret Roberts
na kuhudumu kama mbunge wa Finchley –London Kaskazini tangu mwaka 1959
hadi 1992.
No comments:
Post a Comment