Monday, April 08, 2013

Chadema kuwasha moto bungeni, ni kuhusu wanachodai 'utendaji usiofaa' wa Bunge.

Wakati Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho, Kamati Kuu ya Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulibana Bunge kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na Spika na wasaidizi wake.
 
Pia wabunge hao wameitaka Serikali kuweka wazi mikataba iliyoingia hivi karibuni na Serikali ya China ili wananchi waweze kufahamu kilichomo vinginevyo watatumia kambi hiyo kuwabana wahusika.


Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8, mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.

Kambi ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa kwa hoja binafsi za baadhi ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Maji), James Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari, ambaye hoja yake ilihusu utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Kamati Kuu ilibaini kwamba matukio yaliyotokea katika kikao 10 yalitokana na meza ya spika kutofuata kanuni.


“Tumeamua kwamba Kambi ya Upinzani Bungeni itashughulikia tatizo hili la upindishwaji wa kanuni za Bunge ili wahusika wabanwe kwa vitendo wanavyovifanya,” alisema.

Alisema kambi hiyo itafanya hivyo kwa kufuata sheria na miongozo ambayo inawabana watendaji hao wa Bunge ili waweze kuwajibishwa kwa vitendo vyao.


Akizungumzia mikataba, Mnyika alisema kamati hiyo ina wasiwasi kuhusu mikataba 17 iliyoingiwa na Serikali za Tanzania na China na kutaka iwekwe hadharani.

Baadhi ya mikataba iliyotiwa saini ni katika kilimo, sekta ya afya, miundombinu ikiwamo mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, ujenzi wa Reli ya Kati na ya 

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), kwenda maeneo mbalimbali nchini hali itakayorahisisha usafirishaji wa mizigo.

Mikataba mingine ni uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa cha tumbaku na kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania zana za kufanyia kazi.

“Kamati Kuu inaitaka Serikali kuweka wazi mikataba hiyo vinginevyo watataka ufafanuzi katika kikao cha Bunge la Bajeti kinachotarajia kuanza rasmi kesho.

Kuporomoka kwa maghorofa
Mnyika alisema jopo la wanasheria wa chama hicho, wanafanya uchunguzi wa kuangalia maghorofa yaliyowahi kuanguka na hatua zilizowahi kuchukuliwa.
Alisema ingawa kuna watu ambao wamekuwa wakifikishwa mahakamani, lakini vigogo wengi wamekuwa hawawajibishwi kwa matukio yanayotokea.

“Tukikamilisha uchunguzi huo, tutalitumia Bunge kuwabana wahusika ili wawajibishwe kwa vitendo vyao vya kushindwa kusimamia sheria za ujenzi na kusababisha maafa,” alisema.
Kuteswa kwa Kibanda

Kamati hiyo imesikitishwa na kutekwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda na huku polisi wakiwa hawachukui hatua zinazotakiwa.
Alisema tukio hilo linafanana na lile la kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa madaktari, Dk Steven Ulimboka na mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi.
Mnyika alisema uchunguzi wa matukio hayo unatia mashaka na kwamba kumekuwa na usiri katika uchunguzi unaofanywa na polisi na hivyo Kamati Kuu inataka kuingilia kati ili kubaini ukweli.

Ufisadi bandari
Mnyika alisema katika Bunge lijalo watawasilisha vielelezo bungeni vinavyoonyesha namna Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alivyotoa zabuni ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam kwa Kampuni ya Jitegemee Trading Company Ltd inayodaiwa kuwa ya CCM, kinyume na taratibu.
Madiwani wa Chadema
Mnyika alisema kumekuwa na madiwani wengi ambao wanakamatwa na polisi kwa makosa ambayo hayaeleweki.    

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...