Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA )
jana Jumamosi Aprili 7, 2018 limetoa tamko lenye mambo saba, likiwemo la
kupinga uamuzi wa Serikali kuwafuta kazi watumishi wake wenye elimu ya
darasa la saba.
Akisoma tamko hilo mbele ya wajumbe wa baraza kuu
la TUCTA katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika mkoani Morogoro
mwenyekiti wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema uamuzi huo wa Serikali si
sahihi na hivyo wametaka watumishi hao kurejeshwa kazini.
Amesema baraza limesikitishwa na uamuzi wa kuwaondoa kazini watumishi wa umma na taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini.