Ripoti
iliyoandaliwa kwa hisani ya umoja wa mataifa imeelezea kuwa oparesheni
za kulinda usalama za shirika hilo zinahitaji kufanyiwa mabadiliko
makubwa.
Ripoti hiyo imekusanywa baada ya madai kutolewa hivi
karibuni dhidi ya vikosi vya umoja huo vya kulinda amani kwamba baadhi
wamekuwa wakiwanyanyasa kingono watoto wadogo.
Miongoni mwa
mapendekezo ya ripoti hiyo ni kuwa nchi ambako maafisa husika wanatoka,
zisikubaliwe kuchangia tena wanajeshi katika vikosi vya umoja wa
mataifa.
Pia ripoti hiyo inasema kuwa wanajeshi waliotajwa
kuhusika na uovu huo wanastahili wakabiliwe na sheria, na nchi zao pia
zinafaa kushurutishwa kueleza wazi ni hatua zipi za adhabu
zilizochukuliwa dhidi yao.
Pendekezo jingine lililotolewa katika
ripoti hiyo ni kuwa madai yote ya unyanyasaji wa ngono yanastahili
kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa chini ya miezi sita.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.