Sunday, June 07, 2015

BARCELONA YAWACHAPA JUVENTUS 3-1

http://jambotz8.blogspot.com/p/blog-page_26.html
Barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Hata hivyo Alvaro Morata alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.
http://jambotz8.blogspot.com/p/blog-page_26.html
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.

Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...