Tuesday, June 09, 2015

WATOTO KUNUFAIKA NA DAWA MPYA ZA ARV

Dawa za sasa zinaelezwa kuwa na ladha nzuri kuliko zinazotumiwa hivi sasa
Watoto walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa za kupunguza makali.

Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...