Kocha mkuu wa Yanga Hans Pluijm.
Kocha
mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema wana ari ya kushinda mechi yao ya
mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Etoile du Sahel licha ya kuwaacha
wachezaji wake tegemezi katika msafara wao wa Tunisia.
Yanga
imeondoka Dar es Salaam Jumatano usiku huku wachezaji wake tegemezi,
wakiwemo Hassan Dilunga, Salum Telela na Danny Mrwanda, aliyekuwa
akicheza soka la kulipwa nchini Vietnam wakiachwa kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kifamilia. “Yanga imesajili zaidi ya wachezaji 20, wote ni muhimu katika timu”.
“Ni
kweli niliwahitaji katika mechi yetu ngumu dhidi ya Etoile, lakini
sababu mbalimbali zimepelekea kuachwa kwao”, amesema Pluijm. Yanga
itacheza na wenyeji wao, Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya
raundi ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika
mechi iliyochezwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Yanga
ililazimishwa sare ya 1-1 hivyo kuwa na kibarua kigumu cha kushinda
ugenini huku wenyeji wao wakililia sare ili kucheza hatua inayofuata. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.