Tuesday, March 24, 2015

DAVID CAMERON: AWAMU MBILII ZATOSHA...!!!

David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei. David Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri kuchaguliwa.

Chama kikuu cha upinzani cha Leba kimemshutumu Bwana Cameron kwa kuonyesha uzembe na kushinikiza muhula wa tatu, kwa chama chake cha Conservative, hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KAVUMBAGU: UWANJA ULITUKWAMISHA TANGA

 

Mabeki wa Coastal Union wakiwahani mpira na wachezaji waAzam wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ,Tangajuzi.Azam ilishinda 1-0.

Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu amesema walihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja dhidi ya Coastal Union ila walikwamishwa na uwanja mbovu wa Mkwakwani na kushindwa kuonyesha kiwango chao cha juu.

Mechi hiyo iliyochezwa juzi ilimalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa Azam na kuendelea kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya pointi moja dhidi ya Yanga wenye 37.

Bao pekee la Azam lilifungwa na mshambuliaji wao, John Bocco, na Kavumbagu alilazimika kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Gaudence Mwaikimba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CANNAVARO ATAKA MABAO MENGI YANGA

 Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro
 
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanafunga mabao mengi na kutoruhusu bao katika kila mechi watakayocheza kama wana nia ya kuipokonya ubingwa Azam FC.
Cannavaro alisema katika kipindi hiki ambacho Yanga na Azam FC zinaeendelea kushindana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kitu pekee kinachotakiwa ni kufunga mabao mengi ili mwisho tofauti ya mabao inaweza kuamua bingwa.
Cannavaro alisema kwa hatua ambayo ligi imefikia ni lazima kila mchezaji apambane kuhakikisha timu inamaliza ikiwa bingwa na si vinginevyo kwani malengo yao msimu huu yalikuwa ni kutwaa taji.
“Inapotokea nafasi ya kufunga tunatakiwa tufunge pasipo kuangalia kuwa mfungaji ni beki, kiungo au mshambuliaji. Pia wakati wa kujilinda inatakiwa kila mchezaji ashiriki kuzuia na kulinda magoli, hapo tunaweza kuwa mabingwa bila wasiwasi.
Njia nzuri zaidi ya kuonyesha hilo ni angalau kufunga mabao mawili kwenye kila mechi mpaka mwisho wa msimu,” alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema ushindi walioupata dhidi ya Mgambo JKT juzi Jumapili, umerudisha morali ya kikosi chao kuelekea mechi za mwishoni mwa ligi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MOICT YA KENYA WAIBUKA MABINGWA WA NETIBOLI

Raisi wa TFF Jamal Malinzi
Michuano ya netball ya Afrika ya Mashariki imemalizika Zanzibar huku timu ya MOICT ya Kenya ikitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kuifunga timu ya NIC ya Uganda kwa mabao 32-29.

NIC ndio walikuwa mabingwa watetezi baada ya kulinyakua kombe hilo mwaka jana katika michuano iliyofanyika Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuandaa michuano hiyo mara mbili mfululizo, zamu hii ikiwa ni upande wa Tanzania Zanzibar (visiwani) katika viwanja vya Gymkhana.

Netball, au mpira wa pete ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukihusisha timu za wanawake pekee, lakini katika kuleta usawa (gender balance) kama ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa kikapu (basketball), wavu na mingineyo, mchezo huo katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukishirikisha timu za wanaume katika kuleta hamasa na ushindani.

Kwa upande wa wanaume, wenyeji Polisi ya Zanzibar waliibuka washindi wa michuano hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya kuwafunga wenzao wa JKU (pia ya Zanzibar) kwa mabao 38-34 katika mechi ya vuta nikuvute.

Michuano hiyo hufanyika kila mwaka kwa nchi wanachama kupeana zamu za kuandaa mashindano hayo. Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Zanzibar, Kenya, Uganda na Tanzania Bara. 

Rwanda na Burundi ni sehemu ya jumuiya hiyo ya Afrika ya Mashariki lakini hawana historia kubwa ya kuwa sehemu ya kuwa nchi shiriki. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WANASOKA WA NJE KUPUNGUZWA ENGLAND


Baadhi ya wachezaji wa kiafrika watakaathirika na sheria hiyo.
Shirikisho la kanda kanda nchini England FA sasa linakusudia kuandaa sheria itakayo kupunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika ligi za nchi hiyo.
Mwenyekiti wa shirikisho hilo Greg Dyke asema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua hazitachukuliwa.
Katika mpango pia itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo yote ni ya kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, March 19, 2015

UKAWA WAGAWANA MAJIMBO 211

ukawa
 KAMATI maalumu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), imekamilisha kazi ya ugawaji wa majimbo 211 ambayo ni sawa na asilimia 88 kati ya majimbo yote 239, imefahamika.

Wakati hayo yakiendelea, kamati hiyo imeshindwa kuafikiana katika majimbo 28 ambayo yanasubiri uamuzi wa wenyeviti wa vyama vinavyounda Ukawa, ambao watamaliza kiporo hicho mwezi huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa juu wa umoja huo, kutangaza mkakati wa kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba. Ukawa ni umoja ulioanzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, ukiundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD. 

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo maalumu ya Ukawa, kiliiambia MTANZANIA jana kuwa kwa muda wa wiki moja sasa, kamati hiyo imekamilisha kazi hiyo kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeelezwa linaweza kutoa upinzani mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KIKWETE AWAONYA WANAOHUJUMU KATIBA MPYA

Rais Jakaya Kikwete akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni.

RAIS Jakaya Kikwete ameziagiza mamlaka za ulinzi na usalama kuhakikisha shughuli ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, upigaji kura ya Katiba Inayopendekezwa unafanyika kwa amani na wasioitakia mema nchi wasibadilishe matukio hayo kuwa fujo na kuingiza nchi kwenye vurugu.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua mafunzo elekezi kwa wakuu wapya 27 wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni huku akiwataka kuwa na ushirikiano na vyama vyote vya siasa.

Alisema kazi ya kuboresha daftari la wapiga kura, imeanzia Njombe na itaendelea mikoa mingine na kuwataka viongozi hao kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kukumbusha maana ya kuwa na kitambulisho cha kura ambacho kitamwezesha kupiga kura ya maoni na katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

“Wananchi wasipoteze fursa waone haja ya kujiandikisha na watakaokosa fursa ya kupiga kura hawataipata fursa hiyo tena. Tunataka Watanzania wenye sifa washiriki kikamilifu kuhimiza wananchi wajiandikishe, na kupiga kura,” alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WAMILIKI WA MABASI WACHARUKIA NAULI...!!!

WAKATI wadau wa usafiri nchini wakipendekeza kushuka kwa nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani, wamiliki wa mabasi wametishia kufuta utaratibu wa kutowatoza nauli askari na kuongeza kuwa, hata nauli pungufu za wanafunzi sasa zitakuwa historia.

Wadau wamependekeza kupunguzwa kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani kwa viwango vya kati ya asilimia 15 na 25 huku wakitaka nauli za daladala zipungue kutoka Sh 400 hadi Sh 300 kwa njia ya umbali wa kilometa 10.

Hayo yaliibuka jana wakati wa mkutano wa wadau kukusanya maoni kuhusu mapitio ya viwango vya nauli za mabasi ya mikoani na daladala kupungua kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WANAZUONI WA KIISLAMU WAJIBU HOJA YA MAASKOFU

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Khamis Mataka akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wa taasisi hiyo kuhusu Mahakama ya Kadhi, kuli ni Sheikh Mohamed Id

Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imejibu hoja zilizotolewa wiki iliyopita na Jukwaa la Wakristo nchini kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na hali ya usalama na amani ya nchi.

Machi 10, mwaka huu maaskofu kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania walitoa tamko na kuwataka waumini wao kuipigia kura ya hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu imepatikana kwa njia za hila na kibabe, jambo ambalo sasa limesababisha mvutano.
Katika tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), 

Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, maaskofu hao walisema uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ni uvunjifu wa Katiba na kuwa unahatarisha amani ya nchi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

FDLR TISHIO MASHARIKI MWA DRC

 Wapiganaji wa FDLR
Wajumbe wa mashirika ya kiraia wa vijiji vya Tama na Itala kusini mwa tarafa la Lubero jimboni kivu kaskazini, wanasema kutishiwa na kundi la waasi wa kihutu toka Rwanda wa FDLR kundi wanao ongozwa na Kanali Kizito.

Vitisho hivyo vinakuja kutoka uchapishaji wa ripoti wa mashirika ya kiraia katika sekta hio inayo bainisha hali ya harakati makundi ya waasi na wanamgambo katika maeneo hayo ambao wanahusika naunyanyasaji dhidi ya raia.

Baadhi ya wanachama wa vyama vya kiraia katika vijiji vya Tama na Itala wanasema kua raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali ya mafichoni kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi wanao hishi maeneo hayo hasa FDLR huku wakisema nawaishi kwa tabu wakilala usiku misituni. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MARCHI 19, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAN CITY WATOLEWA LIGI YA MABINGWA

Barcelona na Manchester city
Timu za England zimetolewa katika kinyang'anyiro cha michuano klabu bingwa barani Ulaya,baada ya Man City kuchabangwa bao 1-0 dhidi ya Barcelona na kuondolewa katika mashindano hayo, ilikuwa zamu ya Manchester City kufuata nyayo za waingereza wenzao kutupwa nje ya mashindano na miamba ya soka ya Hispania Barcelona. Katika kipute hicho kilichopigwa katika dimba la Nou Camp.

Wenyeji Barcelona walijipatia bao lao katika dakika ya 31 baada mchezaji Ivan Rakitic kuitumia vema pasi maridadi kutoka kwa Leonel Mess. Hadi mwisho wa mchezo Barcelona 1 Man City hawakupata kitu na kufanya jumla ya matokeo kuwa ni 3-1 baada ya mchezo wao wa awali vijana wa Manuel Pellegrini kuanguka nyumbani kwa jumla ya mabao 2-1.

Na huko nchini Ujerumani vijana wa Jurgen Klopp Borussia Dotmund, ilikiona cha moto baada ya kutandikwa bao 3 kwa mshangao dhidi ya Juventus ya Italia,katika mtanange huo uliopigwa katika dimba la Sigunal Iduna Park, mchezaji Carlos Tevez ndiye aliyepeleka msiba kwa Wajerumani hao kwa kutumbukiza kimiani mabao mawili. 

Dakika tatu tu za mchezo huo zilimtosha Tevezi kufunga bao la kuongoza kabla ya Morata kuandika bao la pili dakika ya 70 na kisha Tevez kutikisa tena nyavu katika dakika ya 79. Matokeo ya jumla kati ya timu hizo mbili yanakuwa ni 5-1 baada ya Juventus kushinda 2-1 katika mchezo wa awali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Wednesday, March 18, 2015

BAADA YA VURUGU KUDUMU KWA SIKU TATU MFURULIZO, HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA TUNDUMA LEO MCHANA

  Wakinawa uso kufuta moshi wa mabomu.

Mkazi wa Tunduma ambae jina lake halikufahamika mara moja akionyesha bomu la machozi ambalo halijatumika alilomnyang'anya askari na kukimbia nalo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

NYALANDU AMJIBU KINANA; 'SASA NITAZURURA ANGANI KUPAMBANA NA MAJANGILI'

 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akielekezwa kitu na wataalam wa ndege hiyo aliyozindua jana.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alionekana kumpiga kijembe Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana aliposema kuwa sasa atakuwa anazurura angani.
Nyalandu alitoa kauli hiyo Dar es Salaam alipozindua ndege nyepesi (Micro-Light, 5H – Hel), ambayo itatumika kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selous.
“Karibuni wote, leo tunazururia hapa uwanja wa ndege na ninazindua ndege hii nyepesi ambayo imetengenezwa Ufaransa, itatumika kupambana na majangili katika Mbuga ya Selous.
“Kwa maana hiyo sasa tunaanza kuzururia angani kupambana na majangili na nasisitiza kwamba ndege hii ni mpya kabisa na gharama za uendeshaji wake ni ndogo kwa vile inatumia petroli,” alisema.
Hivi karibuni Kinana akiwa ziarani mkoani Arusha alimsifia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kuwa ni mchapakazi lakini Waziri Nyalandu ni mzururaji.


Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo ya kupambana na ujangili, Nyalandu alisema imetengenezwa kwa gharama ya Dola za Marekani 2,040,000 na ina uwezo wa kubeba askari mmoja na rubani.


Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo imeundwa kwa usalama wa hali ya juu kwa kuwekewa puto (parachute) ambalo litatumika kushuka chini iwapo ndege itaishiwa mafuta angani.


“Itakapoanza kutumika itasaidia kuwabaini majangili, inakwenda kwa mwendo mdogo iwapo angani hali ambayo inawezesha kuwaona majangili na kila kinachoendelea ardhini kwa wepesi,”alisema Nyalandu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UBUNGE WA ZITTO WANING'INIA...!!!

Zitto Kabwe 

Kitendo cha kutupiana mpira kati ya Ofisi ya Bunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu hatima ya Zitto Kabwe, kimeufanya ubunge wa mbunge huyo kuendelea kuning’inia huku mwenyewe akitazamiwa leo kueleza anachoita ‘maamuzi magumu’.

Kutupiana mpira kulijitokeza jana baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema Bunge linasubiri taarifa rasmi ya kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kutoka NEC, ambayo hata hivyo, nayo ilisema inasubiri taarifa kutoka Chadema huku chama hicho kikisema kinashughulikia kwanza kesi zinazowakabili wanachama wake wanaotuhumiwa kumpiga aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa.
Wakati Makinda akieleza hayo, taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mbunge Zitto zilieleza kuwa leo ataibuka bungeni kwa nia ya kuwaaga wabunge kama alivyoahidi wiki iliyopita. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...