Kumekuwa
na shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga katika hoteli moja mjini
Mogadishu nchini Somali ambapo maafisa wa Uturuki walikuwa wakijiandaa
kumlaki rais Recep Teyyip Erdogan.
Takriban raia watatu wa Somali
waliuawa wawili kati yao wakiwa maafisa wa usalama wakati gari lililojaa
vilipuzi lilipogonga lango la hoteli.
Uturuki hatahivyo imesema
kuwa hakuna mjumbe wake aliyejeruhiwa na kwamba ziara ya rais Erdogan
itaendelea kama ilivyopangwa siku ya ijumaa.
Kundi la wapiganaji wa Alshabaa limesema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.