Friday, December 26, 2014

KIJANA AKAMATWA KWA KUMTUKANA RAIS

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki 
 
Polisi nchini Uturuki wamemkamata mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka kumi na sita kwa tuhuma za kumtukana Rais Recep Tayyip Erdogan.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo alipelekwa mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana Erdogan na chama chake tawala cha AK kwa vitendo vya rushwa wakati wa mkutano wa hadhara katikati ya mji wa Anatolia.
Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ametetea kukamatwa kwa mwanafunzi huyo akisema ofisi ya rais lazima iheshimiwe.
Kumtukana mkuu wa nchi ni makosa kwa mujibu wa sheria za Uturuki na mwanafunzi huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka minne jela endapo atapatikana na kosa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

INDONESIA WAKUMBUKA TSUNAMI

Wanawake eneo la Aceh wakifanya sala ya kukumbuka maafa makubwa yaliyosababishwa na tsunami miaka kumi iliyopita nchini Indonesia 
 
Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, tsunami na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirini katika eneo kubwa.
Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha Sumatra.
Mji huo ulisambaratishwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi na mawimbi ya tsunami. Makamu wa Rais wa Indonesia(Jusuf Kalla) anaongoza maadhimisho hayo na atawashukuru wafanyakazi wa kujitolea katika eneo hilo na duniani kote kwa kulisaidia eneo la Aceh kurejea katika hali ya kawaida baada ya mkasa huo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

ASKARI WATATU WA AU WAUAWA SOMALIA

Askari wa Somalia wakiangalia mabaki ya magari katika moja ya mashambulio ya kigaidi mjini Mogadishu, Somalia. 
 
Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia limesema askari wake watatu na kandarasi raia wameuawa katika shambulio lililofanyika katika makao yake makuu mjini Mogadishu.
Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema wapiganaji wa al-Shabab waliingia katika kambi wakivalia sare kama askari wa jeshi la serikali ya Somalia.
Taarifa hiyo imesema washambuliaji watano waliuawa na wengine kadha kukamatwa. Pamoja na kutoa eneo hilo kuwa makao makuu ya majeshi ya kulinda amani ya AU nchini Somalia, eneo hilo lililoimarishwa pia makao ya balozi za Uingereza na Italia. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA LEO

 Kikosi cha timu ya Azam ya Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania 
  
Ligi kuu ya Tanzania bara, maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom inaanza rasmi mzunguko wa pili leo, Ijumaa baada ya kusitishwa tangu Novemba 7, 2014.
Hadi ligi hiyo ilipositisha mzunguko wa kwanza, tayari timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo zilikuwa zimecheza michezo saba kila moja.

Timu ya Simba ya ligi kuu ya Vodacom
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania, TFF, Simba ambayo ni miongoni mwa timu kongwe za ligi hiyo na ambayo katika mzunguko wa kwanza haikuwa na matokeo mazuri baada ya kwenda sare mara sita na kushinda mchezo mmoja na kujikusanyia pointi tisa ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo, leo inaikaribisha Kagera Sugar inayoshikilia nafasi ya tano katika pambano litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Michezo mingine itafanyika katika viwanja mbalimbali kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii.

Wachezaji wa timu ya Yanga
Mpaka sasa Mtibwa Sugar ndiyo inayoongoza ligi hiyo ya Vodacom baada ya kujikusanyia pointi 15, ikifuatiwa na Young Africans(Yanga) kwa kuwa na pointi 13 sawa na Azam mabingwa watetezi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WENGER AMUWINDA BEKI WA REAL MADRID

Sergio Ramos wa Real Madrid.Kocha wa Arsenal adaiwa kummezea mate 
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewasiliana na ajenti wa beki wa Real Madrid Sergio Ramos kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na kilabu hiyo ya uwanja wa Emirates.
Ramos mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na kilabu hiyo ya Los Blancos kwa takriban muongo mmoja baada ya kuwasili kutoka sevilla kwa kitita cha pauni millioni 20 mwaka 2005.
Hatahivyo ripoti za hivi majuzi zimedai kwamba Ramos huenda akaondoka katika kilabu hiyo ya Santiago Bernabeu baada ya mazungumzo ya kandarasi yake mpya kugonga mwamba.
Na kulingana na mwandishi Esteban Manolete wa AS ,mkufunzi huyo wa The Gunners amewasiliana na wawakilishi wa Ramos ili kuona iwapo anaweza kumvuta mchezaji huyo katika eneo la London kazkazini.
''Wenger amewasiliana na Rene Ramos ajenti na ndugu ya Sergio Ramos'',mwandishi huyo alikimbia kipindi cha La Goleada.
Wenger juma hili alikiri kwamba safu ya ulinzi ya Arsenal haina uongozi baada ya kufungwa bao la dakika za mwisho na liverpool na hivyobasi kupata sare ya 2-2. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Thursday, December 25, 2014

JAMBO TZ BLOG INAWATAKIA WATU WOTE KHERI YA CHRISTMAS

 Heri ya X-mass kwa wadau wote wa blog hii. Tafadhari usisahau ku-like page yetu ya facebook ya Jambo Tz.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

UKAWA WATAKA KICHWA CHA MUHONGO...!!!

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. 

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umelitaka Bunge kuiwajibisha Serikali ikiwa Rais Jakaya Kikwete atashindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ikiwamo kumng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wakizungumza hapa jana, viongozi hao walisema endapo Rais atashindwa kumwajibisha Profesa Muhongo, basi wabunge wao watawasilisha hoja na kushawishi wengine kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na umoja huo utaitisha maandamano nchi nzima.
Mwenyekiti mwenza wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba alihoji kwa nini Rais Kikwete anasita kumwondoa Profesa Muhongo wakati Bunge lilishatoa maazimio.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

UKAWA WATAKA SHERIA YA MAADILI INAYODHIBITI MAOVU

Viongozi wa Ukawa.

Viongozi wa UKAWA

VYAMA vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vimetaka sheria ya maadili itungwe upya ili kuweka uwazi wa watu wote kuona taarifa ya mali za viongozi.

Vyama hivyo vinaamini hatua hiyo, itasaidia wananchi wote kujua mali halisi za viongozi na pia itasaidia kupunguza ufisadi, kutokana na wananchi kutambua ukweli wa mali za viongozi wao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hatua zinazostahili kuchukuliwa, kutokana na suala la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

VIJIJI 45 KUPATA UMEME MARA

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema vijiji 45 mkoani Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Alisema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara, lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti, ililenga kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili, viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini. 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

CHENGE, NGELEJA KUADHIBIWA NDANI YA SIKU 21 ZIJAZO

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti bungeni, Andrew Chenge


Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow wataondolewa katika nyadhifa zao ndani ya siku 21 zijazo, imeelezwa.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola utafanyiwa kazi mapema mwakani.

“Hilo litatekelezwa wakati wa Kamati za Bunge ambazo zitaanza mwishoni mwa wiki ya pili ya Januari mwakani kwa kamati husika kuchagua wenyeviti wapya.”

Wenyeviti hao ni wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, William Ngeleja wa Katiba, Sheria na Utawala na Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC07568
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KESI YA MH. NASSARI YAAHIRISHWA

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari  

Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari jana iliahirishwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Maji ya Chai, Ndikilo Mbise kutokana na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, David Mwita kuwa safarini.
Akiahirisha kesi hiyo, Mbise alisema itatajwa tena Januari 20 mwakani.Mbise alisema Hakimu Mwita amepata msiba, hivyo amekwenda nyumbani kwao mkoani Mara huku, hakimu mwingine wa mahakama hiyo akiwa likizo.
Mbise alisema ameahirisha kesi na kuipangia tarehe nyingine kwa kuwa ni mlinzi wa amani wa eneo hio.
Katika kesi hiyo, Nassari ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo kutokana na kuwa safarini, anatuhumiwa kuchoma bendera ya CCM Desemba 15, saa 11 jioni katika eneo la Maji ya Chai. Bendera hiyo yenye thamani ya Sh250,000 ilikuwa mali ya Raphael Moses.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana ya wadhamini watatu ya Sh1.5 milioni kila mmoja. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

FILAMU YENYE UTATA YAWEKWA MITANDAONI

Filamu ya the Interview iliozua utata 
 
Kampuni ya Sony Pictures imesema kuwa sinema yenye utata ya ucheshi kuhusu namna ya kumuuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, imewekwa katika mitandao Nchini Marekani.
Kampuni hiyo inasema kuwa imechagua njia ya kusambaza sinema hiyo kupitia mitandao ya digitali, ili kuruhusu watu wengi zaidi kutizama sinema hiyo iitwayo, 'The Interview'.
Uzinduzi wa awali wa filamu hiyo ulizingirwa na utata wa mashambulizi ya kimitandao ambapo Marekani ililaumu Korea Kaskazini kwa hitilafu hiyo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

MAREKANI: IS HAIKUANGUSHA NDEGE YETU

 Wapiganaji wa IS wakibeba mabaki ya ndege waliodai kuidungua huko Syria 
 
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamesema kuwa waliidungua ndege ya jeshi la muungano ,lakini Marekani inasema kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kuwa hilo si kweli.
Jordan ni miongoni mwa mataifa manne ya kiarabu yaliopo katika muungano wa majeshi yanayoungwa mkono na Marekani ambayo yameanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa IS.
Ndege hiyo aina ya F-16 ni ndege ya kwanza ya jeshi hilo la muungano kupotea katika maeneo yanayodhibitiwa na IS tangu mashambulizi yaanze mnamo mwezi Septemba.
Rubani wa ndege iliodaiwa kudunguliwa na wapiganaji wa IS akamatwa
Picha za IS zinamuonyesha rubani wa ndege hiyo akikamatwa. Wamemtaja rubani huyo kuwa Moaz Youssef al-Kasasbeh. Wakati huohuo Jordan imesema kuwa hasara iliyopata ya kupoteza ndege yake moja ya kivita, katika anga linalodhibitiwa na waasi wa Islamic State, haitayumbisha majeshi yake kuendelea kukabiliana na matendo ya kigaidi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MARUFUKU YA EBOLA YATOLEWA SIERRA LEONE

Maafisa wa afya wakibeba miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola nchini Sierra leone taifa hilo limetoa marufuku ya siku tatu kazkazini mwa taifa hilo ili kukabiliana na ebola. 
 
Serikali ya Sierra Leone imetangaza siku tatu za marufuku kaskazini mwa taifa hilo, ili kuruhusu jitihada za kukabiliana na kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Msemaji wa serikali amesema kuwa maduka na masoko yatafungwa na hakuna magari ya abiria au pikipiki zitakubaliwa kwenye barabara za eneo hilo.
Sherehe za makanisa kuadhimisha sherehe za siku ya Krismasi pia zimepigwa marufuku.
Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa pakubwa na ugonjwa huo wa ebola. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...