Wednesday, September 24, 2014
MMILIKI WA ALIBABA ATARAJIRIKA ZAIDI
Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha ya Hurun.
Bw.Ma
ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi nchini Uchina kwa mali ya
takriban dola bilioni 25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group Wang
Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika orodha hiyo,
wanamiliki kampuni za mitandaoni huku wakiwabwaga wale wanaomiliki mali
isiyohamishika ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha hiyo.
Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye
wengine walio katika orodha hiyo ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa
intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin Li na pia mwanzilishi wa
soko la mtandao la JD.com, Richard Liu Qiangdong.
Bw Liu ambaye
kampuni yake ilihusika katika ubadilishanaji wa hisa huko New York hapo
Agosti mwaka huu, aliorodheshwa katika nafasi ya kumi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
JESHI LABADILI KAULI KUHUSU WANAFUNZI WALIOTEKWA
Jeshi
la Nigeria limekanusha taarifa ya awali kuwa baadhi ya wanafunzi wa
shule waliotekwa nyara kutoka Chibok na wapiganaji wa Boko Haram,
wameachiliwa.
Msemaji wa jeshi nchini Nigeria, Meja Generali Chris
Olukolade, ameambia BBC kuwa wanawahifadhi wasichana kadhaa lakini
akakana kuwa wasichana hao ni baadhi ya wale waliotekwa nyara na
wapiganaji wa Boko Haram kutoka Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na Boko Haram kutoka shule ya mabweni Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno.
Utekaji
nyara huo ulisababisha ghadhabu kote nchini Nigeria na duniani kote
kiasi cha kusababisha kampeini ya kutaka kuokolewa kwa wasichana hao
kwenye mitandao ya kijamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MHUBIRI ABU QATADA AACHIWA HURU
Mhubiri
muisilamu mwenye utata ambaye alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013,
Abu Qatada, ameachiliwa huru nchini Jordan baada ya mahakama kutompata
na hatia.
Alikuwa ametuhumiwa na kosa la kuhusika katika njama ya kupanga mashambulizi ya kigaidi ambayo ilitibuliwa mwaka 2000.
Jopo
la majaji waliokuwa katika mahakama hiyo, hawakumpata na hatia yoyote
bwana Qatada kutokana na madai kuwa alihusika na njama hiyo ya ugaidi.
Uamuzi
huo umetolewa baada ya Abu Qatada kutopatikana na hatia mwezi Juni
katika kosa lengine la kupanga njama ya mashambulizi mwaka 1998 nchini
Jordan.
Abu Qatada alitimuliwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka
2013 kwa madai ya kueneza itikadi kali Uingereza ikitaka afunguliwe
mashitaka nchini Jordan. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
JAJA AFUTA KESI YA OKWI FIFA
Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na mshambuliaji Genilson Santos ‘Jaja’ kimefanya uongozi wa Yanga, kutupilia mbali wazo la kumshitaki Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa( Fifa).
Tangu aliposajiliwa na Yanga, Jaja ameonyesha
kiwango cha juu cha ufungaji mabao akiwa amefunga mabao manne katika
mechi sita alizocheza hadi sasa katika michuano mbalimbali.
Jaja aliwasahaulisha Wanayanga kabisa habari za
Okwi wakati alipofunga mabao mawili ya ufundi wa hali ya juu katika
mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam walioshinda 3-0.
Kwa mujibu wa taarifa ilizolifikia gazeti hili,
zinasema kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya wanasheria na
baadhi ya wanachama wa Yanga wamemshauri mwenyekiti wao Yusuf Manji
kuachana na jambo hilo kwa sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Monday, September 22, 2014
MATOKEO YA LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND JANA HAYA HAPA
ENGLAND: Premier League | |||||||||||
05:30 | Finished | Leicester | 5 – 3 | Manchester United | |||||||
05:30 | Finished | Tottenham | 0 – 1 | West Brom | |||||||
08:00 | Finished | Everton | 2 – 3 | Crystal Palace | |||||||
08:00 | Finished | Manchester City | 1 – 1 | Chelsea |
MANCHESTER UNITED YAPIGWA 5-3 BILA HURUMA
Cambiasso akishangilia goli alilofunga dhidi ya Manchester United katika uwanja wa The King Power
MANCHESTER United wakicheza ugenini wametandikwa mabao 5-3 dhidi ya Leicester.
Magoli ya wenyeji yalifungwa na Ulloa (2), Nugent, Cambiasso na Vardy.
United walijipatia magoli yao kupitia kwa Van Persie, Di Maria na Herrera
Radamel Falcao akisalimiana na nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney na Ander Herrera kabla ya mechi kuanza.
Katika mechi nyingine iliyomalizika jana jioni, Tottenham wakiwa nyumbani wamepigwa 1-0 na West Brom.
Muda huu
mechi mbili zinaendelea ambapo Everton wapo nyumbani kuivaa Crystal
Palace, wakati Man City wanachuana na Chelsea katika uwanja wa Etihad. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
SIMBA YABANWA MBAVU NA WAGOSI WA KAYA, YATOKA 2-2…!!!
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba
wamelazimisha sare ya mabao 2-2- na Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika
mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika jana jioni uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba chini ya kocha Patrick
Phiri walianza mpira wakilishambulia mara kadhaa lango la Coastal na
katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza Mnyama aliandika bao la
kuongoza kupitia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo mkongwe,
Shaaban Kisiga ‘Malone’.
Katika kipindi hicho cha kwanza,
Simba waliendelea kucheza vizuri kuanzia safu ya kiungo ambapo Piere
Kwizera na Kisiga walionekana kupiga pasi za uhakika, lakini haikuwa
rahisi kupasua ngome ya Coastal.
Mara kadhaa Singano na Chanongo
walipiga krosi kutoka pande zote za kulia na kushoto, lakini Amissi
Tambwe na Okwi walishindwa kukaa maeneo sahihi.
Mnamo dakika ya 36, Tambwe
aliandika bao la pili kwa njia ya kichwa akiunganisha krosi iliyochongwa
na Okwi kutoka winga ya kulia na kumuacha kipa wa Coastal Union
Shaaban Kado akiokota manyoya.
Dakika ya 56, Uhuru aliingia akitoke benchi kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo.
Phiri alifanya mabadiliko ambapo katika dakika ya 64 Tambwe alikwenda benchi na nafasi yake ilichukuliwa na Paul Kiongera. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Thursday, September 18, 2014
SCOTLAND YAAMUA KUHUSU MUUNGANO
Wapiga
kura wamekuwa wakielekea kwa vituo vya kupigia kura katika maeneo mbali
mbali nchini Scotland, ambapo watu wanaamua leo ikiwa wataendela kuwa
sehemu ya uingereza au wawe taifa huru kwa mara ya kwanza kabisa tangu
zaidi ya miaka 300 iliyopita.
Mwandisi wa bbbc anasema kuwa siku
ya leo inatarajiwa kuwa ya shughuli nyingi katika historia ya kupiga
kura eneo la Scotland ikiwa asilimai 97 ya watu wamejisajili kupiga
kura.Kumekuwa na kampeni kali katika saa 24 zilizopita huku ikidhihirika matokeo yanaweza kwenda upande wowote.
Kiongozi wa chama cha Scotish National Party, Alex Salmond, ametaja kampeni ya kuitisha Uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza kama tukio muhimu zaidi la kidemokrasia kuwahi kutendeka nchini humo.
Kadhalika amesema tayari limebadilisha mfumo wa maisha eneo la Scotland.
Idadi kubwa ya wapiga kura wamesajiliwa na kwa mara ya kwanza vijana wenye umri wa miaka 16 na 17 wataruhusiwa kupiga kura. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
POLISI WADAIWA KUTESA RAIA NIGERIA
Polisi
nchini Nigeria wamedaiwa kuwatesa wanaume na wanawake pamoja na watoto.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la
Amnesty International.
Shirika hilo limechapisha ripoti yake
ambayo inadai kwa watu huzuiliwa kinyume na sheria Kaskazini Mashariki
mwa Nigeria ambako jeshi la serikali linapambana na wanamgambo wa Boko
Haram.Serikali ingali kujibu tuhuma hizo.
Shirika hilo linasema kuwa jeshi la Nigeria pamoja na polisi hutumia mbinu tofauti kuwatesa watu ikiwemo kuwapiga, kuwadunga misumari na kuwang'oa meno, ubakaji na dhuluma nyinginezo za kingono.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanajeshi huwatesa watu zaidi katika eneo la Mashariki ambako vita dhidi ya Boko Haram ni vikali zaidi.
Shirika hilo linasema kuwa kati ya watu efu tano na elfu 10 wamekamatwa tangu mwaka 2009 na kunyongwa katika kambi za wafungwa.
Ripoti hiyo yenye mada, "Welcome to hell fire", inatoa taswira mbaya sana kuhusu haki za binadamu kote nchini Nigeria, na inasema kuwa vituo vingi vya polisi vina afisaa wa polisi anayesimamia mateso na kutaka watu kulipa hongo ili kukwepa mateso hayo.
Licha ya kuharamisha mateso, shirika la Amnesty linasema kuwa wanasiasa nchini humo bado hawajapitisha sheria inayowachukulia hatua wale wanaohusika na mateso dhidi ya raia wasio na hatia. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Friday, September 12, 2014
OSCAR HATIANI KWA KUMUUA MPENZI WAKE BILA KUKUSUDIA
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya
Akitoa
uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo
alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango
wake wa choo akiw akatika hali ua mshtuko akidhani kuwa jambazo alikuwa
amevamia nyumba yake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa
kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp nw akutekeleza
mauaji hayo kwa kusudi.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MTOTO ALIYEZAMIA NDEGE NA KUTUA ZANZIBAR UTATA MTUPU
Polisi Zanzibar wameanza
uchunguzi kubaini mazingira ya safari tata ya mtoto Karine Godfrey
aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ndege bila tiketi
wala kugundulika.
Mtoto huyo, Karine au Jenipher Godfrey anayesoma
darasa la tatu katika Shule ya Msingi Jitihada, Dar es Salaam alionekana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Septemba
Mosi saa 11.30 jioni, akieleza kuwa aliingia Zanzibar kwa ndege ambayo
hata hivyo, haikufahamika mara moja ni ya shirika gani.
Alikutwa uwanjani hapo akijiandaa kuondoka kwenda mahali asipopajua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam
Khamis alisema mbali ya kushangazwa na mazingira ya safari ya mtoto
huyo, polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar
wanalifanyia kazi suala hilo.
“Ni
jambo la kushangaza. Tunajiuliza, huyu mtoto
alifikaje katika ndege bila ya kuwa na tiketi wala taarifa zozote
kuelezea safari yake na je, huko Dar es Salaam aliondokaje hadi kuingia
katika ndege bila ya hivyo vitu, sielewi ilikuwaje. Kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
CHEYO AWAVAA UKAWA BUNGENI, ADAI HAWAKUKUBALIANA NA RAIS KULIVUNJA BUNGE...!!!
Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), John Cheyo amewavaa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akieleza kuwa walichokubaliana katika kikao chao na Rais Jakaya Kikwete ni kwamba Bunge liahirishwe Oktoba 4 na si kama wanavyodai wakiwa nje.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Cheyo
alisema hakuna makubaliano ya kutaka Bunge lisitishwe kabla ya
kukamilisha kazi zake Oktoba 4, ikiwamo kutoa Katiba itakayopendekezwa
kwa wananchi.
“Mojawapo tulilokubaliana ni Bunge hili lipate
Katiba itayopendekezwa kwa wananchi,” alisema Cheyo huku akipigiwa
makofi na kelele kutoka kwa baadhi ya wajumbe.
“Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda
tulionao, haiwezekani mchakato mzima ukamalizika na maana ya kumalizika
mchakato ni kura ya maoni ya wananchi na ndiyo wenye Katiba.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)