WEKUNDU wa Msimbazi Simba
wanaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 30 mwaka huu.
Simba wamepiga kambi visiwani
Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri
akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya
taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na
kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.
Simba ilianza programu ya mazoezi
mara moja kwa siku hapo jana katika fukwe za bahari ya Hindi, lakini
Phiri ameamua kuongeza dozi ambapo leo atafanya mazoezi mara mbili,
(asubuhi na jioni).
Lengo la Phiri ni kupata muda wa
kutosha wa kusuka kikosi chake akijua wazi kuwa msimu ujao atakumbana na
changamoto kubwa ya kusaka ubingwa wa Tanzania bara.
Pia kocha huyo alisisitiza suala
la mechi za kirafiki ili kukiona kikosi chake kwa mara ya kwanza na
kujua nini cha kufanya zaidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz