
Rwanda imekuwa ikiendedesha harakati za upatanishi na pia kuwakumbuka waliokufa katika mauaji hayo
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari
nchini Rwanda Emmanuel Mbarushimana amekataa uendeshwaji wa kesi yake na
mahakama ya Kigali kwa kutoa pingamizi kwamba hana haki zilizo sawa na
mwendesha mashitaka.
Mshukiwa huyo alikabidhiwa Rwanda na nchi ya
Denmark mapema mwezi wa saba mwaka huu ili kujibu mashitaka ya kuhusika
katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.Mushukiwa huyo Bwana Emmanuel Mbarushimana amesema kesi yake haiwezi kusikizwa hadi pale atakapopata haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka. Hoja yake ilikuwa kwamba ni lazima na yeye aruhusiwe kukaa badala ya kusimama wakati kesi yake ikisikilizwa na wakati huo huo mwendesha mashitaka asimame badala ya kukaa kama ilivyozoeleka.
Aidha, amesema kuwa hajafurahia utaratibu unaotumiwa wa kuingia katika chumba cha mahakama ambapo mwendesha mashitaka na majaji wanaingia kwa kutumia mlango mmoja kinyume na mushitakiwa.
Mwendesha mashitaka amemshitaki kwa kushiriki katika mauaji dhidi ya watutsi yaliyotokea katika maeneo mbali mbali katika mkoa wa zamani wa Butare kusini mwa Rwanda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz