Thursday, August 01, 2013
HUYU NDIYE BINTI ALIEFARIKI KWA KISA KILICHOANZIA FACEBOOK, FAMILIA YAKE KUISHITAKI FACEBOOK?

Kampuni
ya mtandao wa kijamii wa facebook imezungumza baada ya tukio la yule
msichana aliejiua kutokana na kisa ambacho kilianzia facebook January
2013.
Kumbe Chanzo ni picha ambayo ilikua inamuonyesha
mrembo huyu wa Italia Carolina akiwa amelewa, aliiweka kwenye page yake
ya facebook ambapo mpenzi wake wa zamani kwa kushirikiana na marafiki
walianza kumtolea maneno machafu Carolina, walimtukana hivyo yeye na
mdogo wake wa kike wakaamua kuripoti facebook lakini hakuna hatua zozote
zilizochukuliwa.
Kwenye mji wa Italia wa Novarra ndio tukio
lilitokea kupitia facebook na likaingia mpaka kwenye maisha ya Carolina
ambapo bila yeye kujua, tukio liliendelea kuwa kubwa na kutishia kuwa
kubwa kumshinda.
MWANAJESHI AMGONGA RAIA BAADA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KATIKA MATAA YA KUONGOZEA MAGARI ENEO LA TAZARA DAR ES SALAAM

Gari lililomgonga raia likipita katika upande wa kulia zinakotokea gari
za Buguruni,Ubungo,baada ya dereva kukiuka sheria za usalama barabarani.

Raia aliyegongwa akiwa hoi baada ya kugongwa na dereva wa gari la Jeshi akipepewa na askari Jeshi.

JUMA KASEJA APATA DILI KUBWA KONGO...!!!
![]() |
| Mlinda mlango wa Taifa Stars Juma Kaseja |
NAHODHA wa timu ya soka
ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Juma Kaseja amesema kwamba
amefanya mazungumzo tu na wakala wa klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini bado hajaingia Mkataba na klabu
hiyo ya Lubumbashi.
Akizungumza jana mchana,
Kaseja amesema kwamba mtu aliyejitambulisha kwake kama wakala wa Lupopo
alimfuata wakafanya mazungumzo na kufikia makubalino juu ya dau la
usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.
Hata hivyo, kipa huyo
namba moja Tanzania amesema kwamba baada ya mazungumzo hayo na
maafikiano, wakala huyo amepeleka majibu Lupopo ambao wakiafiki ndipo
masuala ya Mkataba yatafuatia.
MUSWADA WA SUALA LA KODI YA SIM CARD KURUDISHWA BUNGENI AGOSTI

Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya NIPASHE na HabariLeo matoleo
ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya
simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria
ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti
kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.
Wiki
iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha
Wamiliki wa Kampuni za Simu - TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)
Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu
kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa
mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178
zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa
2013/14 kutokana na kodi ya simu.
VYAKULA VYA MAFUTA NI CHANZO CHA KUKUKOSESHA USINGIZI

Tumekuwa tukipokea maoni toka kwa watu wengi juu ya matatizo ya kukosa usingizi, ingawa kuna sababu nyingi zinazoweza kukufanya ukose usingizi kama magonjwa nk, ila mlo nao ni moja ya sababu hizo.Na moja ya vyakula hivi ni vile vyenye mafuta (fat) mengi kama burger, chipsi nk. Tafiti zinaonesha kuwa, vyakula hivi sio tu hukufanya uongezeke uzito bali pia huabiri mfumo wa kulala.
Tafiti zinaendelea kuwa, vyakula hivi vizito huamsha mfumo wa usagaji vyakula (digestion system) na kuifanya ianze kufanya kazi, hii hukupelekea mwili wako kuwa hai na pia hukufanya mara nyingi kujisikia kwenda haja hivyo kukukosesha usingizi.
Hivyo basi epuka kula mlo wenye wanga mwingi wakati wa usiku au angalau kwa masaa mawili kabla ya kwenda kulala.
Wednesday, July 31, 2013
MWANASHERIA KUISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU KRISTO...!!

Maajabu
mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano
kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee .
Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki
serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu
Kristo .
Mwanasheria
huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The
Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na
Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria
huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa
kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya
Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia
yoyote ya kustahili adhabu hiyo .
Dola
Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa
Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo
Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo
mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua
Bwana Yesu .
FAHAMU KWANINI UNATAKIWA KUZIFANYA NDIZI KUWA SEHEMU YA MAISHA YAKO.
Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana
karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa
tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako
kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku
moja .Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako .
Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kujikinga na maradhi kadhaa.
MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU MWAKA WA MASOMO 2013/2014 HAYA HAPA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr Shukuru kawambwa.
---
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa
kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la
wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.
Kati
ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A)
na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.Wanafunzi 363
wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma
elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
---
MAELEKEZO MUHIMU:
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.
ZIDANE AWAFUNGUKIA SPURS, AWATAKA WAMPE NAFASI YA KUCHEZA REAL MADRID KUTIMIZA NDOTO ZAKE
Gareth Bale alipokuwa akiwasili uwanja wa Heathrow akitokea Hong Kong baada ya kupata majeruhi
Hakuna
tabasamu: Bale, anaweza kuwa mchezaji ghali zaidi duniani akimzidi
Ronaldo kama dili la usajili wake wa pauni milioni 85 litakamilika
kwenda Real Madridi, lakini wakati akiwasili London alionekana kuwa na
mawazo mengi kichwani mwake.
Zidane
alisisitiza kuwa : “Kama mchezaji ameonesha nia ya kujiunga na Madrid,
basi Tottenham wampe ruksa ya kuzungumza na sisi. Nafasi ya kuichezea
Real Madrid huwa inatokea mara moja katika maisha ya mchezaji na
inaeleweka kuwa Gareth Bale hataki kukosa nafasi hii muhimu”.
AFYA YA MANDELA YAZIDI KUIMARIKA

RAIS mstaafu nchini Afrika Kusini , Nelson Mandela aliyelazwa hospitalini tangu tarehe nane mwezi Juni, anaonyesha dalili za afya yake kuimarika.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali. Hata hivyo Mandela mwenye umri wa miaka 95 angali hali mahututi ambayo inadhibitiwa na madaktari.
Rais Jacob Zuma amewataka watu kuendelea kumuombea Mandela na kuwashukuru wale waliotenda mema kwa niaba ya Mandela. (HM)
Mandela ambaye ni rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa.
Alifungwa jela miaka 27 baada ya kuanzisha vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Anajulikana na ukoo wake kwa jina Madiba, na alichaguliwa kama rais wa Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya wazungu kumaliza utawala wao na kisha akaondoka mamlakani baada ya miaka mitano ya kutawala nchi.
Katika taarifa yake, bwana Zuma alitoa wito kwa wafanyabiashara kuunga mkono mradi unaofadhiliwa na wakfu wa Mandela kujenga hospitali ya watoto.
"Madiba anapenda sana watoto, na anawatakia afya nzuri. Anatutaka tuhakikishe kuwa wanaishi maisha mazuri katika siku za baadaye,'' alisema Zuma.
Wakfu wa Mandela , ungependa kujenga hospitali yenye uwezo wa kuwashughulikia watoto 238 wa kulazwa pamoja na kuwatibu watoto kote nchini Afrika Kusini. Chanzo: bbcswahili
UN: VIFO VITOKANAVYO NA HIV VYAPUNGUA AFRIKA

UMOJA wa Mataifa umetangaza kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi Mashariki na Kusini mwa Afrika vimepungua kwa asili mia 40.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS umehusisha hatua za sasa na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi. (HM)
Umoja wa Mataifa umesema mataifa ya
Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu
wanaokufa kwa ukimwi kwa zaidi ya nusu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005. Chanzo: bbcswahili
Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005. Chanzo: bbcswahili
Tuesday, July 30, 2013
KANISA KATOLIKI PAROKIA YA URU LAKUMBWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA

HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina.
Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.
Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
“Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.
Subscribe to:
Comments (Atom)





