Thursday, August 01, 2013

MUSWADA WA SUALA LA KODI YA SIM CARD KURUDISHWA BUNGENI AGOSTI

Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya NIPASHE na HabariLeo matoleo ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.

Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Simu -  TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)  Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178 zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 kutokana na kodi ya simu.

Kodi hizo za Shilingi 1,000 kwa mwezi ambazo Waziri Dk Mgimwa akiwasilisha makaridio ya mapato na matumzi kwa Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2013/14 Bungeni mwezi Juni tarehe 13, mwaka hu, alisema:

  1. Zilianza kutozwa na serikali mwanzoni mwa Julai, mwaka huu hivyo kuwalazimu wamiliki wa simu nchini kuingia gharama zaidi kwa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato. 

  2. Serikali inakusudia kutoza ushuru kwenye huduma zote za simu za mkononi, kama chanzo kipya cha mapato ya  badala ya muda wa maongezi peke yake.

  3. Asilimia 2.5 ya mapato ya kodi hiyo yatatumika kugharimia elimu nchini kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali.

  4. Inaanzishwa kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi ambazo zitakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa Wakala wanaotoa huduma hizo kupitia simu za mkononi.

  5. Mapendekezo hayo ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali. 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...