Kampuni
ya mtandao wa kijamii wa facebook imezungumza baada ya tukio la yule
msichana aliejiua kutokana na kisa ambacho kilianzia facebook January
2013.
Kumbe Chanzo ni picha ambayo ilikua inamuonyesha
mrembo huyu wa Italia Carolina akiwa amelewa, aliiweka kwenye page yake
ya facebook ambapo mpenzi wake wa zamani kwa kushirikiana na marafiki
walianza kumtolea maneno machafu Carolina, walimtukana hivyo yeye na
mdogo wake wa kike wakaamua kuripoti facebook lakini hakuna hatua zozote
zilizochukuliwa.
Kwenye mji wa Italia wa Novarra ndio tukio
lilitokea kupitia facebook na likaingia mpaka kwenye maisha ya Carolina
ambapo bila yeye kujua, tukio liliendelea kuwa kubwa na kutishia kuwa
kubwa kumshinda.
Kati ya saa tisa au nane usiku Carolina alijirusha
kutoka kwenye dirisha la chumbani kwake gorofani nyumbani kwao na
akaangukia kichwa, kichwa ndio kilitangulia kutua kwenye sakafu ya zege
ambapo baada ya kufariki ilipatikana barua aliyoiandika maalumkwa
wanaomtesa…. aliandika ‘“mmefurahi sasa? mmeniumiza vya kutosha?
mmepata kisasi mlichokuwa mnatafuta?“
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba mwendesha
mashtaka Mahakamani Novarra anaangalia uwezekano wa kuishtaki kampuni ya
facebook kwa kushindwa kuziondoa kauli chafu zilizokua zimeandikwa
kwenye wall ya Carolina ambazo ndio zilipelekea kujiua.
Hata
hivyo facebook wamezungumza kuhusu hicho kifo kwa kusema
“tumesikitishwa na tukio la kifo cha Carolina, mioyo yetu na mawazo yetu
yako kwa familia yake na marafiki zake , unyanyasaji wa aina yoyote ile
hauna nafasi kwenye facebook na siku zote tumekuwa tukiwasisitiza
vijana na wazazi kutoa ripoti za matukio kama haya, tunatoa maneno yote
ambayo yanaenda kiunyume na sheria na sera yetu”
Na Millard Ayo
Na Millard Ayo