Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Catherine
Kieu, mwenye miaka 50, alipatikana na hatia ya mashitaka ya kutesa na
kosa la kuharibu viungo vya mwili katika shambulio la Julai 11, 2011 na
kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini anaweza kufikiriwa kupewa
msamaha baada ya kutumikia miaka saba.
Alitiwa hatiani Aprili kwa kila kosa moja la kutesa na kuharibu viungo vya mwili.
Muathirika, anayefahamika kama Glen wakati wote wa kesi, alikuwa mahakamani kwa ajili ya hukumu ya jana.
"Natumaini
hii itakuwa mara ya mwisho kabisa ninayoweza kumwona," alisema Glen.
"Najihisi nafuu kiasi fulani, na ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwangu."
Muathirika huyo alikimbizwa hospitali, lakini upasuaji kurejesha uume wake haukufanikiwa.
Wakati
wa kesi hiyo, muathirika huyo mwenye umri wa miaka 60 alitoa ushahidi
kwamba uume wake hauwezi tena kuunganishwa mahali pake na kwamba anahisi
kama ameuawa.
Kieu
alikuwa na wivu na hasira kuhusu mipango ya mumewe kumpa talaka sababu
alimwona rafiki yake wa zamani wa kike, upande wa mashitaka ulisema.