RAIS
Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais
Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma,
aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji
Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha
mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka
na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza
ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo
wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu
imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili.
Kamati
Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa
za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na
Wazanzibari.