Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa
Na Steven KanyephAfisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa ametoa takwimu ya ufaulu kwa elimu ya msingi na sekondari kwa muda wa miaka mitatu kwa mkoa wa shinyanga katika kikao cha taarifa ya elimu kwa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa uliopo mkoani Shinyanga , siku ya jana.
Akitoa takwimu hizo kwa elimu ya msingi Bi. Lopa amesema kuwa matokeo ya elimu ya msingi yamekuwa ya yakipanda mwaka hadi mwaka , na kwa mwaka 2010 yalikuwa ni asilimia 42.5 wakati mwaka 2009 yalikuwa asilimia 31.9 mwaka 2011 matokeo yalikuwa asilimia 44.2 hivyo kuwepo na ongezeko la asilimia 1.7% kwa mwaka 2009 hadi 2011 wakati mwaka 2012 wanafunzi waliofauru ni asilimia 56.1% sawa na ong ezeko la asilimia 11.9
Afisa elimu huyo ameainisha sababu zilizopelekea ongezeko la ufaulu huo kwa mwaka 2012 kwa elimu ya msingi kwa mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa viongozi wa elimu ngazi za wilaya na mkoa , ufuatiliaji wa ufundisha ji, ongezeko la walimu kutoka uwiano wa 1.74 hadi 1.54 na ongezeko la vitabu kwa wanafunzi kutoka uwiano wa f1.6 hadi 1.4