Tuesday, June 18, 2013

BANANA ZORRO KURUDI KWENYE GAME KWA KISHINDO

 
Msanii na mmiliki wa Band ya B-band Banana Zorro amefunguka kuwa kimya kingi siku zote kina mshindo na kueleza kuwa alikuwa kimya kwa sababu alikuwa busy na kazi za Band lakini kwa sasa anatarajia kudodosha ngoma nyingine siku za karibuni kwa wale fans wake kaeni mkao wa kura. Banana amefunguka hayo leo alipokuwa katika Show ya Kikaangoni Live inayofanyika kila siku ya Ijumaa kupitia Accounts za Facebook za Eatv na East Africa Radio ambapo mashabiki wake wanapata nafasi ya kuuliza maswali na yeye kuwajibu. 
Moja ya shabiki aliuliza akitaka kujiunga katika B-band afanyaje na jibu lilikuwa anapaswa kufanya mazoezi ya kutosha na akiwa teyari awasiliane na meneja wake Allan Lucky na mambo yatakuwa poa.
Akizungumzia moja ya fanikio aliyopata katika Muziki ni pamoja na kumiliki Band yake mwenyewe ambayo ni B-band ambayo inaendelea kukuwa kila siku na kufanya vizuri pia.

CATHY WA BONGO MOVIE ALIA NA USHIRIKINA ULIPO NDANI YA TASNIA HIYO....AWATAKA WASANII WAMRUDIE MUNGU

Mwigizaji wa Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’  naye amenyanyua kinywa chake na kuonesha jinsi gani anakerwa na wasanii wanaoshinda kwa waganga ili kutafuta ustaa.
Akiongea na mwandishi  wetu hivi karibuni, Cathy alisema kuna baadhi ya wasanii (hakuwataja majina) wamekuwa na tabia za kuzunguka kwa waganga wakitafuta kuwa juu katika tasnia ya filamu suala ambalo halipendezi na kuwasihi wawe na hofu ya Mungu.

“Vifo vya wasanii vimetokea vingi sana, nilidhani kutokana na vifo hivyo wangepata hofu ya Mungu na kuacha mambo yasiyofaa vikiwemo vitendo vya kishirikina lakini hawakomi, wananikera sana. Ipo siku wataumbuka kwani Mungu siyo binadamu,” alisema Cathy.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 18, 2013

.
.

Monday, June 17, 2013

HIZI NI ISHARA ZINAZOSEMEKANA KUWA NI ZA MAFREMASONS...!!!


 





MKASA MZIMA KUHUSU KUPIGWA KWA MBUNGE NASSARI KATIKA KITUO CHA KURA MAKUYUNI



Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.

"Lakini tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni...

"Huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani...

"Baada ya hapo,tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,

"Hata tulipofika huko waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta Nassari. Tulivyoona hivyo, tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi."

Taarifa zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari walimpiga dereva wake Gadi Palangyo na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas Kilongola, hadi walipokuja kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Makuyuni.

Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.

GERALD HANDO WA CLOUDS FM NUSURA AFUMULIWE NA BASTOLA LEO


Habari na Salute 5

PICHA ZA MH. FREEMAN MBOWE AWATEMBELEA MAJERUHI NA WAFIWA WA BOMU LILILOLIPUKA SOWETO JIJINI ARUSHA

DSC09341Mwenyekiti wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto, wakati wa zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.
DSC09327
Mhe.Mbowe na Mhe. Lema wakishauriana jambo..

DSC09343Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo lilishamabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari la matangazo lina majeraha mawili katika mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.

VIONGOZI NA WAZAZI WAASWA KUFICHUA UOVU DHIDI YA WATOTO

(Picha na maktaba)
Na Mwandishi Wetu Steven Kanyeph.
Viongozi wa serikali kwa kushilikiana na wazazi wametakiwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika wanapoona watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili unyanyasaji wa kijinsia, ukeketaji na kuozeshwa katika umri mdogo.

Hayo yamesemwa na mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye ni mkuu wa wilaya ya kishapu bwana; Willson Mkambaku kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya shule ya msingi Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Bwana Mkambaku amewataka viongozi na wazazi washilikiane kwa pamoja kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya unyanyasaji, ubakaji .ulawiti , na kuhakikisha kuwa watoto wanaendelezwa kielimu kushiriki katika maamuzi , ikiwa ni pamoja na kukomesha ajira kwa watoto.

Aidha watoto waameitaka jamii kwa kushirikiana na viongozi kupiga vita imani potofu zenye kuleta madhara kwa watoto kama vile ukeketaji ,ndoa za lazima, uasherati , mauaji ya vikongwe ,albino pamoja na madawa ya kulevya.,

Madhimisho ya siku ya mtoto wa afrika hufanyika kila mwaka tarehe 16 mwezi wa 6 lengo ni kukumbuka mauaji ya kikatili ya mamia ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto afrika ya kusini mwaka 1976 baada ya watoto kufanya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Kauli mbiu ya madhimisho hayo kwa mwaka huu ni KUONDOA MILA ZENYE KULETA MADHARA KWA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE

WABUNGE WA CHADEMA WAGOMA KUINGIA BUNGENI KUFUATIA BOMU LA ARUSHA...IGP ATOA NAMBA YAKE KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA


Wakati Jeshi la Polisi nchini limesema limepata taarifa za mwonekano wa mtu aliyetupa bomu katika mkutano wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Arusha,Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema wabunge wake leo hawataingia bungeni.
 Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mbowe alisema wabunge hao watawasili Arusha kwa ajili ya kuungana na wananchi pamoja na wanachama kwenye msiba huo.
Alisisitiza kwamba kuanzia leo mahema yatawekwa viwanja vya Soweto kwa ajili ya kuomboleza msiba huo na  mara polisi wakimaliza uchunguzi wao na kutoa majibu juu ya vifo hivyo, marehemu hao watasafirishwa.
Wakati Mbowe anatoa kauli hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza jana mjini Arusha na waandishi wa habari, alisema taarifa za awali zinaonesha mlipuko huo ni bomu la kutupwa kwa mkono (grumeti)  na hivi sasa timu ya wataalamu  ikiongozwa na Kamishna wa Operesheni Maalumu wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Naye  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema  katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ameahidi kupambana na kuhakikisha wahusika wanapatikana.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 17, 2013

.
.

Sunday, June 16, 2013

BINTI ACHOMWA MOTO HADI KUFA BAADA YA KUOMBA AOLEWE NA NDUGU YAKE...!!!


Msichana wa miaka 19 amechomwa moto hadi kufa na mama yake kupigwa baada ya kuwaomba wazee wa kijiji kuruhusiwa kuolewa na mvulana mmoja kutoka kijijini hapo na ukoo mmoja, polisi wa India wamethibitisha.
Anju Yadav, kutoka kijiji cha Karahkol, wilayani Deoria katika jimbo la Uttar Pradesh, alichomwa moto nyumbani kwake wakati mama yake, Gyanwati Devi, mwenye miaka 48, alipokuwa upande mwingine wa kijiji hicho akiiomba halmashauri ya kijiji kumruhusu Anju aolewe na rafiki yake wa kiume aliyekuwa na mahusiano naye kwa miaka miwili, Ranjit Yadav, mwenye miaka 21.
Lakini halmashauri ya kijiji hicho, sambamba na baba wa mvulana huyo, Jai Hind Yadav, mwenye miaka 52, walitupilia mbali maombi hayo wakisisitiza ilikuwa kinyume cha utamaduni.

Badala yake, baba wa mvulana huyo alikimbilia kwenye nyumba ya familia na kumchoma moto msichana huyo, ilidaiwa.
Jamii ya India inafahamika mno kwa mfumo wake wa ukoo ulioingiliana, ambao unaweza kuzuia watu kutoka jamii tofauti kuoana na katika baadhi ya matukio kuafikiana na jambo kama hilo.

OMMY DIMPOZ AANZA SAFARI YA KWENDA NYUMBANI KWA AKINA MANGWEA KUOMBA MSAMAHA

 
Kutokana na kauli aliyotoa msanii Ommy Dimpoz ya SITAKUFA KIJINGA NA KIMASIKI KAMA KAMA ALIVYOKUFA NGWAIR, hii ndio kauli aliyotoa baada ya mashabiki na Wanamuziki wenzake kumaind kwa kile alichokisemahttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKiN6BrFwokEV_2Z_ENfiFrWaNHdg_4ahM2D2NktQGeixKbh3-1ZjbVuKvlJtAk_l3af9FSyxVZYQkdxlXT1WMaz8T3v94BhpaRuUlze-iL1pPiQyA46yUL0_lSrcBCqYLWDnMLuwMKZw/s1600/dimpoz.jpg
NANUKUHU:
"Samahani tena sana sitawacha kuomba msamaha, nimekubali makosa na hivi sasa naelekea nyumbani kwao kuomba msamaha kwa familia na nitue kwa vituo vya radio kuomba msamaha kwa wabongo na wote niliowaudhi. Samahani sana na nakubali mimi si mtu bila nyinyi na sikuongea kuhusu legend Ngwair kwa ila mbaya. One love". mwisho wa kunukuu

KIM KARDASHIAN AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE...!!!

NI siku ya furaha kwa Kanye West! Kim Kardashian amejifungua mtoto wa kike Jumamosi asubuhi katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center, Los Angeles, mtandao wa OMG umethibitisha.

Inasemekana Kardashian, 32, alikuwa na West pembeni mwake wakati wa kujifungua, kumkaribisha duniani binti yao mwezi mmoja kabla ya muda uliotarajiwa. Tarehe halisi ya kujifungua ilitazamiwa kuwa Julai 11.

"Kim aliugua Ijumaa usiku na hatimaye kupata mtoto mapema," chanzo cha hospitali kimeileza Us Weekly. “Inafurahisha, wote katika hali nzuri!"

Kanye West, 36, na Kim - wote wawili wakiwa ndo mara ya kwanza kuwa wazazi, wamekuwa wapenzi tangu Aprili 2012. Desemba 30, 2012, West alitangaza kwamba mpenzi wake alikuwa na mimba wakati wa tamasha lake Atlantic City.

"Simamisha muziki na wote mpige kelele kwa mama kijacho," alisema West jukwaani akionyesha kidole kwa Kim ambaye alikuwa mmoja wa  watazamaji.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 16, 2013

.
.

HABARI YA KINA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA


Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.


Mama akikimbizwa hospitali kupata matibabu.

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...