Msichana
wa miaka 19 amechomwa moto hadi kufa na mama yake kupigwa baada ya
kuwaomba wazee wa kijiji kuruhusiwa kuolewa na mvulana mmoja kutoka
kijijini hapo na ukoo mmoja, polisi wa India wamethibitisha.
Anju
Yadav, kutoka kijiji cha Karahkol, wilayani Deoria katika jimbo la
Uttar Pradesh, alichomwa moto nyumbani kwake wakati mama yake, Gyanwati
Devi, mwenye miaka 48, alipokuwa upande mwingine wa kijiji hicho
akiiomba halmashauri ya kijiji kumruhusu Anju aolewe na rafiki yake wa
kiume aliyekuwa na mahusiano naye kwa miaka miwili, Ranjit Yadav, mwenye
miaka 21.
Lakini
halmashauri ya kijiji hicho, sambamba na baba wa mvulana huyo, Jai Hind
Yadav, mwenye miaka 52, walitupilia mbali maombi hayo wakisisitiza
ilikuwa kinyume cha utamaduni.
Badala yake, baba wa mvulana huyo alikimbilia kwenye nyumba ya familia na kumchoma moto msichana huyo, ilidaiwa.
Jamii
ya India inafahamika mno kwa mfumo wake wa ukoo ulioingiliana, ambao
unaweza kuzuia watu kutoka jamii tofauti kuoana na katika baadhi ya
matukio kuafikiana na jambo kama hilo.
Hatahivyo,
inaeleweka kwamba haikubaliki kwa watu kutoka ukoo mmoja na kijiji
kuoana. Ndoa ndani ya Gotra (ukoo) mmoja pia hairuhusiwi katika
utamaduni wa India, hasa katika mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo ambako
makundi ya kiukoo, yanayofahamika kama Khap Panchayats, yanachukulia
ndoa kama hizo kuwa kosa la jinai.
Rakesh
Kumar, mkuu wa Kituo cha Polisi cha Ikauna, alisema: "Jai Hind pamoja
na wanakijiji wengine watatu walikimbilia nyumbani kwa msichana huyo na
kumwagia mafuta na kisha kuchoma moto wakati mama yake akiwa kwenye
kikao hicho cha halmashauri. Tumewakamata wafuasi wawili wa kundi hilo
wakati wengine wawili wakiwa wanaendelea kusakwa."
Anju aliungua asilimia 85 ya mwili wake wote na alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali Alhamisi jioni.
Anju
alikuwa peke yake wakati wanaume hao wanne walipovamia nyumbani kwake.
Katika kuchanganyikiwa aliruka kutoka kibarazani kwake hadi ghorofa ya
pili kujaribu kujiokoa. Alivunjika mikono na miguu yake.
Wanakijiji walimmwagia maji, lakini wakati huo alikuwa tayari amepata majeraha makubwa ya moto.
Mama yake, Gyanwati, alisema wote binti yake na Ranjit walipendana sana na kudhamiria kufunga ndoa.
Gyanwati
alikwenda nyumbani kwa Jai Hind Jumatano jioni kujadiliana kuhusu suala
la ndoa lakini pale yeye na familia hiyo walipokataa alikwenda katika
baraza la kijiji kwa msaada, jambo la kawaida katika India.
Gyanwati
alisema: "Nilitaka kumwona binti yangu akiwa mwenye furaha. Walipendana
mno; sikuwa na tatizo na ndoa yao. Lakini pale nilipokwenda kwa Jai
Hind na maombi hayo alinieleza ni dhambi kuoana ndani ya ukoo mmoja na
hatokubaliana na ndoa hiyo."
Polisi wamethibitisha kwamba Jai Hind bado hajapatikana.
No comments:
Post a Comment