Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani
mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne
na wengine kujeruhiwa.Bomu hilo
lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama
hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika
katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya
wananchi.Hilo ni tukio la pili la
bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu
lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,
Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine
kujeruhiwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.
Mama akikimbizwa hospitali kupata matibabu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.
Watu
walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo
lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema,
wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua
za kumaliza kuhutubia.Taarifa
zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye
eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini
alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa
wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga
risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.Baada
ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika
wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi
wengine wakiwa bado wako jukwaani.Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.Hali
hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia
mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi
hali ambayo ilizidisha taharuki.Baadhi
ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na
watu wengine waliokuwa katika eneo hilo.Miongoni
mwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo la mlipuko wa bomu ni Katibu
wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ambaye amelazwa katika
hospitali ya Selian.Mbowe
akizungumza katika hospitali ya Selian aliwataka wanachama wa chama
hicho watulie kwa sababu tukio hilo ni kubwa na lina mambo mengi ndani
yake.
Alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha kuwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo wanapata matibabu kwanza.
Mbowe aliwataka watu wote waliopotelewa na ndugu kufika katika hospitali zote za mji wa Arusha kutambua ndugu zao waliojeruhiwa.
Alisema Chadema itagharimia matibabu ya watu wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.
Mbowe
alisema chama chake kwa sasa hakiwezi kutoa tamko lolote kuhusiana na
tukio hilo la bomu kwa sababu wanafuatiliwa na baadhi ya askari polisi
na maofisa wa Usalama wa Taifa.
Katika
hospitali ya Selian, Mganga wa zamu, Dk Ekenywa alisema kuwa hospitali
hiyo imepokea majeruhi 25 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.
Waandishi
wa habari walishuhudia baadhi ya wanachma wa Chadena pamoja na viongozi
wao akiwamo Mbowe wakitoa damu kwa ajili ya majeruhi.
Awali
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alihitimisha kampeni kwa
chopa katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli na kukumbana na mkutano
wa kampeni wa CCM uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Edward
Lowassa.
Viongozi
hao, walifanya mikutano katika kata hiyo na kila chama kilitamba
kushinda leo na kuwaondoa wananchi na hofu za kutokea vurugu.
Mbowe
licha ya kufanya mkutano huo, pia alifanya mikutano katika Kata ya
Kaloleni Uwanja wa Soweto mjini Arusha na mamia ya wakazi wa Arusha wa
kata zote nne na mkoani Manyara, katika kuhitimisha kampeni za uchaguzi
mdogo wa udiwani unaofanyika katika kata mbalimbali nchini.
Uchaguzi mdogo wa kata nne za Jiji la Arusha na Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli, unatarajiwa kufanyika leo.
Uchaguzi
wa Kata ya Makuyuni, unafanyika kuziba nafasi ya Diwani wa CCM, Abdilah
Warsama aliyefariki dunia, kata nne za Jiji la Arusha, uchaguzi
unafanyika kutokana na waliokuwa madiwani wa Chadema kufukuzwa uanachama
kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
Vyama
vilivyosimamisha wanaogombea udiwani ni CCM, Chadema na CUF. Kwa upande
wa CCM ni Emanuel Meliali (Kaloleni), Emmannuel Laizer (Elerai), Edna
Jonathan Sauli (Kimandolu) na Victor Mkolwe (Themi) .
Chadema
wanaogombea ni Melance Kinabo “Kaburu” (Themi), Emmannuel Kessy
(Kaloleni), Jeremiah Mpinga (Elerai) na Rayson Ngowi (Kimandolu).
Kwa upande wa CUF waliosimamishwa kugombea ni Abbas Mkindi Darwesh (Kaloleni) John Bayo (Elerai) na Lobora Ndarvoi (Themi).
Kampeni
Kampeni
za uchaguzi huo, mdogo, zilikuwa na upinzani mkubwa na kwa Jiji la
Arusha, wakati Chadema, ilikuwa ikiongozwa na mbunge wa jimbo hilo,
Godbless Lema, CCM iliwatumia vigogo wake wote wa juu wa chama hicho.
Vigogo
hao waliokuwa Arusha ni Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba, Katibu wa
Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,
Abdalah Bulembo.
Wengine
waliokuwa Arusha ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwanri, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen Wassira na wabunge kadhaa
wakiongozwa na mbunge wa Simanjiro, Christopha ole Sendeka.
Kata ya Makuyuni
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema jana kuwa chama
hicho, kina uhakika wa ushindi katika Kata ya Makuyuni na kata nne za
Arusha.
“Tumefanya kampeni kwa amani na utulivu na nina imani ya ushindi mkubwa hasa hapa Makuyuni,” alisema Nangole.
Mbowe katika kata hiyo, jana alifanya mkutano mfupi baada ya kutua kwa chopa, akitokea mkoani Manyara.
Mbowe
aliwataka wakazi wa kata hiyo, wasiwe na hofu wajitokeze kupiga kura
leo. Kwa upande wa Lowassa, ambaye ameweka kambi katika kata hiyo, pia
alitoa wito kwa wakazi wa kata hiyo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura
leo.
Kwa
pamoja viongozi hao ambao walipishana muda mfupi, Mbowe akianza kupita
na baadaye Lowassa kuhitimisha mkutano, kila mmoja alitamba chama chake
kushinda leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nape alisema chama hicho kina imani na ushindi leo na alipongeza kampeni kuwa za amani.
“Tuna imani polisi wataimarisha ulinzi leo,” alisema Nape.
Nape jana jioni, alitarajiwa kuhitimisha kampeni mkoani Manyara.
Lema akizungumza katika mikutano jana, alisema wana imani Chadema itaibuka na ushindi katika kata zote.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment