
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
Mbunge huyo alikamatwa kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyedai kuwa aliwachochea wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea kiongozi huyo na kupopoa gari lake kwa mawe.
Hata hivyo, siku moja kabla ya kukamatwa Lema aliwaonesha waandishi wa habari ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani aliyotumiwa na Mulongo akimtishia kuwa atamfungulia kesi yoyote anayoitaka.
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.









.jpg)












