MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa
Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo ‘Mashauzi’, Jumatano
iliyopita alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa
Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha
shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya
Veronica Tarik.
Chanzo cha habari kituoni hapo
kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake
aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa
Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini
walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.
Veronica aliwakimbiza wawili hao na
kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi
kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali
iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka
kuwadhalilisha.
Baada ya
Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na
kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa
Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.