kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman
Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Mwandishi kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.



















