Wednesday, April 03, 2013
LOWASSA AMTOA KAFARA PINDA
WABUNGE WAUNGANISHA NGUVU KUTAKA KUMSULUBU BUNGENI
RIPOTI
ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka
2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam,
imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa,
Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Pinda
anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka
katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo
vya zaidi ya watu 40.
Kutokana
na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa
ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa
chini ya kiwango.
SUMATRA YATANGAZA KUPANDA KWA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU NA DALADALA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Kaimu
Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari
leo katika makao makuu ya taasisi hiyo wakati akitangaza kupanda kwa
viwango vya nauli ya mabasi ya mikoani na Daladala.
………………………………………………………………..
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha
mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa
mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada
ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama
msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata
kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza
kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.
Tuesday, April 02, 2013
Baada ya kuiponda Cloud's Fm, Lady Jaydee ajipanga kuanzisha Radio yake mwenyewe.....!!!
Hatimaye tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.
Na sasa imebainika kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.
Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Inaonesha kuwa mchakato wa kuanzisha radio hiyo unaenda vizuri kiasi cha kuweka wazi na kuwa hiyo ndio sababu alichukua uamuzi huo wa kuandika mambo ambayo yangeweza kuiharibu career yake ya muziki.
Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Kila lakheri Lady Jaydee. Kwa usimamizi wa mumewe Gadner G Habash ambaye ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya radio, kituo hicho huenda kikafanya vizuri.
source:bongo5
MAAJABU HAYA, BABA AFANYA MAPENZI NA MWANAE WA MIAKA 9 MBELE YA MKEWE
Mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa), amefanyiwa
unyama wa kutisha na baba yake wa kambo kwa kunajisiwa, kulawitiwa na
kulazimishwa kulamba mbegu zake za kiume. Mtoto huyo anayeishi mkoani Pwani, imedaiwa ana hali mbaya kiafya kutokana na kudaiwa kufanyiwa kitendo hicho kwa muda wa miaka miwili. Mwanaume anayedaiwa kufanya unyama huo amefahamika kwa jina la Adam Taliani maarufu kama `Kiredio' (37). Inadaiwa kuwa baba huyo alikuwa akifanya kitendo hicho mbele ya mama wa mtoto huyo ambaye ni mke wake, akiwatishia kuwaua kwa panga kama watatoa siri hiyo. Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa mtoto huyo Chiku Selemani alisema vitendo hivyo alianza kufanyiwa na baba yake wa kambo tangu mwaka 2011 wakati mama yake alipoanza kuishi na mwanaume huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz |
KIJIJI CHA MISUKULE CHAGUNDULIWA NCHINI
Msukule.
Msukule.
Msukule.
Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA
na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa
hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji
hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini
kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa
kimazingara.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
AGNES MASOGANGE AWEKA PICHA INSTRAGRAM AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA
Ni
miezi michache imepita tangu video queen wa bongo Agnes Masogange
aadhirike baada ya video yake chafu kusambaa ikionesha waki**** na jamaa
yake.
Lakini
sasa inaanza kuonekana kuwa dada huyu hii ni michezo yake baada leo
kupost picha zinazomuonesha wakiwa kimahaba na mpenzi wake katika
mtandao wa instragram.JE HIVI TUKIONA VIDEO NYINGINE AKIWA NA HUYU
MCHIZI TUTASHANGAA AU TUTASEMA NDIO KAZI YAKE?
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR ALIGOMBEA UBUNGE TIKETI YA CUF 2010
IMEELEZWA
kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF
ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa,
mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa
uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi
Jimbo la Rahaleo.
“Ni
kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji
ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa
kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Hata
hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na
CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.
Kwa
mujibu wa kumbukumbu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ripoti ya
matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Jimbo la Rahaleo, mgombea wa
CCM, Nassor Salim Ali maarufu kama Jazirra aliibuka na ushindi kwa
kupata kura 3,952 sawa na asilimia 63.10, wakati mgombea wa CUF, Omar
Mussa Makame alipata kura 2,310 sawa na asilimia 39.9 na kushika nafasi
ya pili.
RUNGWE MBEYA IMEENDELEA KUKUMBWA NA MATUKIO YA MAUAJI YA KUTISHA, TAHADHARI PICHA HIZI ZINATISHA.....!!
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZINAZOONEKANA ZA MTOTO AYUBU HAPA NICHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU
|
Rais Jakaya Kikwete Akutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Monday, April 01, 2013
Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema
Mwili
wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa
ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram
asubuhi ya leo
KAMANDA MPINGA MATATANI
ADAIWA KUAMURU GARI LILILOBEBA MAZAO YA MISITU LIACHIWE.
Kutokana na tukio hilo, askari mwenye namba D.9523 Koplo Azizi wa kituo kidogo cha polisi Ikungi mkoani Singida ameingia matatani baada ya kulikamata gari hilo lenye namba za usajili T 271 BTR na trela namba T 686 BTX lenye urefu wa futi 40.
SIMULIZI YA ALIYENUSURIKA KIFO KUTOKA GHOROFA YA 15.
Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi.
FUNDI ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.
Subscribe to:
Posts (Atom)