Hii ni kwa wale wote wapenda kujichora miili
ya kwa inayojulikana kama tattoo
Wednesday, March 27, 2013
UJUMBE WA FIFA KUSIKILIZA WAGOMBEA TFF APRILI 16
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika
kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe huo ambao moja ya shughuli zake
kuwasikiliza wote walioenguliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF
na hawakuridhika na uamuzi huo, utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka
huu.
Kwa mujibu wa barua ya
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar
Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na kutoa ripoti kwa
mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa mwongozo.
Ujumbe huo utakutana na pande mbalimbali
zinazohusika wakiwemo wagombea, kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia
ujumbe huo unatarajia kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi wa viongozi wa TFF ulikuwa
ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya
baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika kuwa hawakutendewa haki na
wangependa shirikisho hilo liingilie kati.
‘Siri ya Kuuawa Zitto Yafichuka’ – Sio Kweli.
Katika
gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna
habari yenye kichwa chenye maneno
‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na
vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa
atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa
kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na
wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja,
sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane
na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu
kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio
tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi
kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela
Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba
mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
TIGO yazindua Ofa ya bei moja kupiga simu kwenda mitandao yote
Meneja
wa Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani
ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi, kushoto kwake
Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma .
Mtaalam
wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda
mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya
nchi.
Albam ya Justin Timberlake yauza kopi 968,000 katika wiki ya kwanza
Albam mpya ya
Justin Timberlake, “The 20/20 Experience” imekamata nafasi ya kwanza
kwenye Billboard 200 chart, kwa kuuza kopi 968,000 katika wiki yake ya
kwanza, kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.
“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.
Mauzo huzo hayo ya “20/20′s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.
Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.
“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.
Mauzo huzo hayo ya “20/20′s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.
Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.
Dk Slaa awatuhumu Usalama wa Taifa
Dar es Salaam.
Kwa ufupi
“Chadema
ni chama makini na hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote wala idara
yoyote inayotumiwa na baadhi ya watu ili kutaka kukizohofisha,” alisema
Dk Slaa ambaye mara kwa mara amekuwa akilalamika kuchezewa rafu.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa
ameanza kuisakama Idara ya Usalama wa Taifa kuwa wanatumia mbinu
mbalimbali kuwahujumu na kwamba mbinu zinazofanywa na idara hiyo ni
kueneza propaganda walizodai za uongo dhidi yao.
Akizungumza jana makao makuu cha chama hicho jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema: “Tumezibaini mbinu zinazofanywa na Usalama wa Taifa kwa kutumiwa na CCM kueneza propaganda za uongo dhidi yao kwa lengo la kukichafua chama, lakini haziwezi kufanikiwa kwani tayari tumegundua mbinu zao.
ROSE NDAUKA: KAJALA AJIPANGE KUTIMIZA NDOTO ZAKE
Habari na saluti5
NYOTA
wa filamu, Rose Ndauka amemzungumzia msanii mwenzie wa filamu, Kajala
Masanja aliyeponea chupuchupu kwenda jela miaka mitano na kusema kuwa,
anachoamini ni kwamba sasa Kajala atajipanga na kuyafanya maisha yake
yaende kama alivyokusudia hatimaye kutimiza ndoto zake.Saluti5
ilizungumza na Rose ili kupata maoni yake juu ya kuachiwa huru kwa
Kajala aliyekuwa jela kwa muda mrefu, ambapo alisema kuwa kikubwa ni
kushukuru mungu kwa kuweza kwake kurudi tena uraini, lakini pia sasa ni
wakati wa kuzijenga upya ndoto zake.
“Binafsi, siwezi kujua
kwa sasa Kajala mwenyewe amepanga kitu gani juu ya maisha yake, lakini
ninaamini atafanya yale anayayowaza katika akili yake, hususan
kuhusiana na kuendeleza mipango yake ya kimaisha,” alisema Rose.
JK: afunga rasmi mafunzo ya JKT ya muda mfupi kwa wabunge RUVU JKT
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy Maro)
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UZALISHAJI JKT RUVU
Mwakilishi
wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala
kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
leo mchana.Wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya MrisWabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete
wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU
leo.Wabunge
walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa
Tuesday, March 26, 2013
SANAMU YA KANUMBA KUWEKWA BAGAMOYO, SOMA STORY HAPA
Of course Steven Kanumba had so much fans
kwenye hii tasnia ya filamu za
Bongo and he could defenetely take ‘Bongomovie’ somewhere far na ndio
maana anakumbukwa kutokana na ku-inspire wengi. Taarifa zisizokuwa rasmi kitaani kwasasa ni kwamba kwenye maazimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha the late steven kanumba mwaka huu huenda ikatengezwa sanamu yenye sura yake na kuwekwa kwenye mji wa kihistoria wa bagamoyo Mkoani Pwani. Muigizaji Stevene Kanumba alifariki mwezi April mwaka jana 2012 nyumbani kwake Sinza Vatkan dar es salaam akiwa na umri wa miaka 28 baada ya majibizano na mpenzi wake Elizabeth Michael ‘lulu’ ambae pia ni muigizaji. |
MCHORO WA KUMUUA ASKOFU MOKIWA
MCHORO uliosanifiwa na watu ambao inaaminika walitaka kumuua Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa ni hatari.
Askofu
Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa.
Taarifa za kila upande,
zinathibitisha kwamba mchoro huo ulisanifiwa kitaalam na kwamba
kilichomwokoa Mokiwa ni Mungu.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.
MCHORO WENYEWE
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.
WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA
Wakati tume ya kuchunguza
matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi,
imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao
isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa
taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa,
wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama
matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa,
wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni
takribani 10,000 na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine
wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani
ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na
kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa,
NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza
kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini,
kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,”
alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake lisiandikwe
gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)