Wednesday, March 27, 2013

TIGO yazindua Ofa ya bei moja kupiga simu kwenda mitandao yote

Meneja wa Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi, kushoto kwake Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma .
Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi.
Tigo Tanzania leo imezindua ofa ambayo inatoa nafasi ya kipekee na thamani kubwa sana kwa wateja wake kuweza kupiga simu kwa gharama nafuu zaidi za kiwango kimoja kwenda mitandao mingine ndani ya nchi kufurahia dakika nyingi zaidi za mawasiliano kuliko ilivyokuwa awali.
Pia, ofa hiyo inatoa fursa kwa wateja wa Tigo kupiga simu kwa mitandao mingine nje ya Tanzania kwa punguzo la 20%.
Kiwango hicho kimoja cha kupiga simu, baada ya kuwezeshwa, kitamwezesha mteja kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa masaa 24 kwa siku saba.
“Tigo inawajali sana wateja wake na inatambua umuhimu wa kuwapatia huduma bora tena kwa gharama nafuu ambayo wataweza kuimudu, na huduma bora ambayo inaendana kabisa na thamani ya fedha zao. Kwa huduma hii ya upigaji simu kwenda mitandao mingine kwa viwango sawa, wateja wetu wa Tigo wataweza kufurahia kupiga simu kwenda mitandao mingine waipendayo kwa gharama nafuu kabisa; sanjari na kupiga simu nje ya nchi kwa punguzo la 20%..” alifafanua Wiliam Mpinga, Meneja Chapa wa Tigo.
Aliendelea kufafanua kuwa, huduma hiyo pia itakuwa mkombozi mkubwa kwa wateja wote wa Tigo ambao wanafanya biashara mbalimbali ama kufanya kazi na makampuni mbalimbali ambapo itakuwa ni fursa nzuri kwao kuwasiliana na wateja wao ndani na nje ya nchi. Vile vile huduma hii itawawezesha wateja wetu kuwa na mazungumzo marefu kwa njia ya simu pasipo bughudha ya aina yeyote.
Bw. Mpinga aliendelea kufafanua kuwa, “Kwa mara nyingine tena tumetoa nafasi nzuri kwa wateja wetu wa Tigo ambao tunawathamini sana kufurahia uhuru wa kuongea kwa muda mrefu na kwa ghrama nafuu, na tunatoa wito kwa wananchi wengine kujiunga na Tigo ili waweze kunufaika na huduma hii.
Kwa huduma hii ya viwango sawa vya kupiga simu kwenda mitandao mingine, tunaoa fursa kwa wateja wetu kumpigia mtu yeyote anayependa, kwa kumpa uhuru wa kuwasiliana na yeyote anapenda..”
Kutumia huduma hii, metja wa Tigo anapaswa kujisajili na huduma ya Time, kisha apige namba *149*90#  ambapo atwezeshwa moja kwa moja kujiunga na huduma hiyo kwa wiki nzima.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...