Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry (wa pili kulia) akipokelewa na
mwenyeji wake Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya
Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) kwa niaba ya Waziri Dkt.
Abdallah Kigoda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndeege wa
Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere jijini Dar. Wa Pili kushoto ni Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou wakielekea katika chumba maalum cha wageni
maalum kwenye Uwanja huo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akibadilishana mawazo baadhi ya
maafisa mbambali wa Wizara.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akizungumza na mwenyeji wake
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Odilo Majengo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry katika tete a tete na Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akipitia moja ya magazeti maarufu
nchini Tanzania la The Citizen ambalo limeandika habari kuhusiana na
mkutano aliokuja kuhudhuria. Kushoto ni Dkt. Alberic Kacou.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akisaini daftari la wageni katika
chumba maalum cha wageni maalum mara baada ya kuwasili nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akiteta jambo na Mkurugeni Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou wakati akijiandaa kuondoka katika
Uwanja wa ndege. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na
Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akiingia kwenye gari maalum kuelekea
hotelini.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akiwasili hotelini na kulakiwa na
baadhi ya maofisa wa WIPO.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property
Organization (WIPO) Francis Gurry akipewa maelekezo machache kuhusiana
na taratibu za mkutano wa kujadili Changamoto za Maendeleo katika Bara
la Afrika katika mkutano nchini Tanzania.Picha Zote na Zainul Mzige wa Mo Blog.
Mkurugenzi
Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry
amewasili nchini Tanzania leo kuhudhuria mkutano utakao zungumzia pamoja
na mambo mengine Changamoto za Maendeleo katika Bara la Afrika.
Katika
Mkutano huo wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho pia wadau
watazungumzia nafasi ya WIPO katika Kuchochea Maendeleo barani Afrika.
Mkutano huo
utakaohitimishwa kesho kutwa utamalizika kwa kwa kuwa na kipindi cha
majadiliano na kutoa maoni, ambapo wadau watatoa mitazamo yao kuhusiana
na ajenda zilizowasilishwa na kutafuta mwelekeo wa pamoja.