Monday, March 11, 2013

WAKATI WABUNGE WAKITESA, MADEREVA WAO WALIA NA NJAA KALI

WAKATI wananchi wengi, wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge nao wameibua kilio chao wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao, walilazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wakilalamikia haki zao kukaliwa na wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Wabunge, Juvenille Joseph.

Pamoja na mambo mengine, barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa kusimamia maslahi yao, hali inayowafanya waishi kwa shida.

Katika barua hiyo, madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya kazi, huku wakitaka posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika akaunti za wabunge.

“Mheshimiwa Katibu wa Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta kwako hoja zetu ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.

“Kwa kipindi chote, madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano ya mdomo baina ya dereva na mbunge.

“Ndiyo maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.


“Tunaomba ofisi yako izingatie kuwa kazi ya ubunge ni ya kipindi cha miaka mitano, bila mkataba ni vigumu kujua suala la haki za kikazi.

“Hivyo basi, tunaomba ofisi yako isimamie kuhakikisha kuwa wabunge wote wanatoa mikataba ya ajira kwa madereva wao,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...