Mkazi wa Tunduma ambae jina lake halikufahamika mara moja akionyesha bomu la machozi ambalo halijatumika alilomnyang'anya askari na kukimbia nalo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz. |
Wednesday, March 18, 2015
BAADA YA VURUGU KUDUMU KWA SIKU TATU MFURULIZO, HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA TUNDUMA LEO MCHANA
NYALANDU AMJIBU KINANA; 'SASA NITAZURURA ANGANI KUPAMBANA NA MAJANGILI'
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akielekezwa kitu na wataalam wa ndege hiyo aliyozindua jana.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alionekana kumpiga kijembe Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana aliposema kuwa sasa atakuwa anazurura angani.
Nyalandu alitoa kauli hiyo Dar es Salaam alipozindua ndege nyepesi (Micro-Light, 5H – Hel), ambayo itatumika kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selous.
“Karibuni wote, leo tunazururia hapa uwanja wa ndege na ninazindua ndege hii nyepesi ambayo imetengenezwa Ufaransa, itatumika kupambana na majangili katika Mbuga ya Selous.
“Kwa maana hiyo sasa tunaanza kuzururia angani kupambana na majangili na nasisitiza kwamba ndege hii ni mpya kabisa na gharama za uendeshaji wake ni ndogo kwa vile inatumia petroli,” alisema.
Hivi karibuni Kinana akiwa ziarani mkoani Arusha alimsifia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kuwa ni mchapakazi lakini Waziri Nyalandu ni mzururaji.
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo ya kupambana na ujangili, Nyalandu alisema imetengenezwa kwa gharama ya Dola za Marekani 2,040,000 na ina uwezo wa kubeba askari mmoja na rubani.
Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo imeundwa kwa usalama wa hali ya juu kwa kuwekewa puto (parachute) ambalo litatumika kushuka chini iwapo ndege itaishiwa mafuta angani.
“Itakapoanza kutumika itasaidia kuwabaini majangili, inakwenda kwa mwendo mdogo iwapo angani hali ambayo inawezesha kuwaona majangili na kila kinachoendelea ardhini kwa wepesi,”alisema Nyalandu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UBUNGE WA ZITTO WANING'INIA...!!!
Kitendo cha kutupiana mpira kati ya Ofisi ya Bunge, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu
hatima ya Zitto Kabwe, kimeufanya ubunge wa mbunge huyo kuendelea
kuning’inia huku mwenyewe akitazamiwa leo kueleza anachoita ‘maamuzi
magumu’.
Kutupiana mpira kulijitokeza jana baada ya Spika
wa Bunge, Anne Makinda kusema Bunge linasubiri taarifa rasmi ya
kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kutoka NEC,
ambayo hata hivyo, nayo ilisema inasubiri taarifa kutoka Chadema huku
chama hicho kikisema kinashughulikia kwanza kesi zinazowakabili
wanachama wake wanaotuhumiwa kumpiga aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu
wake, Dk Willibrod Slaa.
Wakati Makinda akieleza hayo, taarifa kutoka kwa
watu wa karibu wa mbunge Zitto zilieleza kuwa leo ataibuka bungeni kwa
nia ya kuwaaga wabunge kama alivyoahidi wiki iliyopita. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
'KURA YA MAONI IPO PALE PALE'
Kaimu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh. Samuel Sitta.
SERIKALI imesema haiwezi kubadili msimamo wake kuhusu upigaji wa Kura
ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, licha ya kuwepo maoni ya viongozi
wa dini ambao wanataka jambo hilo lisitishwe.
Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta alisema
jana mjini hapa kuwa pamoja na kuwepo kwa tofauti kati ya Jukwaa la
Wakristo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, msimamo wa Serikali uko pale pale.
Sitta, ambaye anakaimu shughuli za serikali bungeni kutokana na
kutokuwepo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema Serikali inakubaliana
na maoni ya Kardinali Pengo kuwa waumini waachwe waamue wenyewe kuhusu
Katiba Inayopendekezwa.
Alisema kama viongozi wa dini wamegawanyika hakuna namna ya kuwafanya
wawe na kauli moja, lakini akasisitiza kuwa jambo la msingi ni kuachwa
kwa mtu aamue mwenyewe aina ya kura atakayopiga.
Hivi karibuni Pengo alitofautiana na Baraza la Maaskofu (TEC) na
Jukwaa la Wakristo ambao wanataka upigaji wa kura ya maoni usitishwe,
kwa maelezo kuwa wananchi hawajapewa muda wa kuisoma na kuielewa katiba
hiyo na kama Serikali itang’ang’ania ni vyema waumini wa kanisa wapige
kura ya hapana. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MAASKOFU WA JUKWAA LA WAKRISTO WAMEKOLEZA MOTO KUIKATAA KATIBA
Gazeti la Mwananchi la Machi 13, 2015 lilibeba
ujumbe mzito kwa Watanzania. Kichwa cha habari kimoja kilisomeka:
“Maaskofu: Pigieni Katiba kura ya hapana.”
Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo ambao ni Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcicius
Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT)
Askofu Daniel Awet, kwa sauti moja wamewataka waumini wao kujiandikisha
kwa wingi katika Daftari la Wapigakura, kuisoma vyema Katiba
Inayopendekezwa na hatimaye kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana.’
Sababu kuu za kuwahamasisha waumini wao na
Watanzania kuikataa Katiba Pendekezwa ni mbili. Mosi ni kulazimisha kura
ya maoni ya katiba mpya kufanyika bila maandalizi ya kutosha, yakiwamo
maridhiano ambayo yameligawa Taifa katika vipande vipande. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
AL SHABAAB YAUA WATU WATATU NCHINI KENYA
Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema kuwa takriban watu watatu
wameuawa katika mji wa kazkazini wa Wajir, yapata kilomita 100 kutoka
mpaka na Somalia. Watu waliofunika nyuso zao walishambulia duka moja na kufyatua risasi, kulirushia magurunedi kabla ya kulichoma.
Kundi
la wapiganaji wa Al-Shabaab limeongeza mashambulizi yake kazkazini
mashariki mwa Kenya katika siku za hivi karibuni ,na kufanya
mashambulizi mawili katika mji wa Mandera ambao una pakana na Somali.
Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa la Somalia la mashambani na limesajili idadi kubwa ya raia Wakenya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
MAKAMU WA RAIS WA S LEONE AFUTWA KAZI
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo. Siku
ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani
kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia
maisha yake.
Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake .
Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana. Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia. Hatahivyo amekana madai hayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
MONACO HAWAKUSTAHILI KUSONGA MBELE
Meneja
wa klabu ya soka ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anaamini timu ya
Monaco haikustahili kusonga mbele kwenye hatua ya nane bora ya ligi ya
mabigwa ulaya.
Licha ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Monaco walishindwa kufuzu kwa nane bora baada ya kupoteza
mchezo wa kwanza kwa kuchapwa 3-1.
Kocha Wenger amesema haamini
kama timu hiyo ilitakiwa kusonga mbele “ukiangalia idadi ya mashuti
yaliyolenga goli utashangaa, kupoteza mchezo kunauma ila hatujapoteza."
Hii imekua ni mara ya tano mfululizo kwa washika bunduki hao wa London kushindwa kufuzu hatua ya nane bora. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SERENA WILLIAMS ATINGA NANE BORA
Nyota wa mchezo wa tenesi Serena Williams ametinga katika hatua ya nane bora ya michuano ya BNP huko Indian Wells. Serena
amefanikiwa kufanya vizuri kwa kumshinda Sloane Stephens anayeshika
nafasi ya 33 kwa ubora wa dunia kwa seti 6-7 (7-3) 6-2 6-2,
Sloane alipoteza mchezo huu baada ya kushindwa kuhimili mikiki miki ya mpinzani wake aliekua anacheza kwa juhudi kubwa.
Williams alikataa kucheza hapo baada ya kufanyiwa vitembo vya kudharauriwa mwaka 2001. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)