Thursday, March 12, 2015
CHEYO AKARIBISHA 'WAGENI' KUWANIA URAIS UDP
Mbunge wa Bariadi Mashariki na
Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo amesema wanakaribisha wanachama
wa chama chochote cha siasa nchini kuwania nafasi ya urais kupitia
chama hicho.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, kiongozi
huyo alisema chama hicho bado hakijateua mgombea urais hivyo milango
iko wazi kwa wanasiasa ambao wako tayari kujiunga na chama hicho kwa
lengo la kuwania urais.
“Hiki chama ni cha watanzania wote hivyo tunatoa
rai kwa mtu yeyote aliye tayari kuwa mwanachama wetu milango ya kuwania
urais kupitia chama hiki ipo wazi’’ alisema Cheyo
Alisema yeye bado hajaamua kuwania nafasi hiyo
kwa sasa muda ukifika atasema lakini kwa sasa ni mapema kutoa tamko
kwamba atawania wadhifa huo.
Aliongeza kwamba anasikitishwa na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) kuwahamasisha watu wasipigie kura Katiba
inayopendekezwa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi.
‘’Raia wote wana haki ya kupiga kura sasa ikiwa
Ukawa wanatembea kila kona ya nchi kuwahamasisha wananchi kuacha
kuipigia kura katiba hiyo ni kosa,’’ alisema Cheyo
Pia Kiongozi huyo wa UDP alisema tume ya uchaguzi
ndio yenye majibu ya mashine zinazotumika kuandikisha wapiga kura
kwenye daftari la kudumu, (BVR) kwamba zinafaa au hazifai.
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya watu
hususan wanasiasa na wasomi wanaojitokeza na kusema mchakato wa
kuandikisha wapiga kura usimamishwe kwa sababu zao mbalimbali . Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
IS WANATUMIA GESI YA KLORINI IRAQ
Shirika la Utangazaji -BBC- limepata ushahidi unaoonyesha wapiganaji wa wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini.
Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq.
Serikali
ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika
mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji
Islamic State katika mji wa Tikrit.
Katika picha video ambayo BBC
imeoneshwa na kikosi cha kuharibu mabomu nchini Iraq imeonekana mlipuko
wa bomu ukiwa na moshi wa rangi ya chungwa ukipaa angani.
Bomu hilo lilikuwa na kiasi kidogo cha Klorini ambayo huenda hutumika kama sumu kwenye maeneo ya wazi.
Kumekuwa na taarifa za wapigani wa Islamic State kutumia gesi ya klorini tangu walipoanza harakati zao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UMOJA WA MATAIFA WALAUMIWA KUHUSU SYRIA
Ripoti
ya mashirika zaidi ya ishirini ya misaada ya kibinadamu na yale ya
kutetea haki za binaadamu yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kwa kushindwa kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria.
Ripoti
hiyo imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa
kushindwa kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia uhuru wa huduma
za misaada ya kibinadamu kwa waathirika.
Ripoti ya masharika hayo ni ya kuadhimisha miaka minne ya vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa.
David
Milband ambaye ni Rais wa Shirika la kimataifa la Uokoaji International
Rescue Committee amesema kuna ongezeko dogo la misaada inayotolewa
kuwasaidia raia wa Syria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
BAYERN MUNICH, PSG ROBO FAINALI UEFA
Timu
ya Bayern Munich ya Ujerumani na Paris St. Germain ya Ufaransa
zimesonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa
barani Ulaya kufuatia matokeo waliyayapata usiku wa kuamkia leo.
Wakicheza
kwa kujiamini Bayern Munich ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali
katika mashandano hayo baada ya baada ya kuwapa kichapo cha mbwa mwizi
wapinzani wao Shakhtar Donetsk ya Ukrine cha magoli 7- kwa mtungi.
Magoli
ya Bayern Munich yalitiwa kimiani na Thomas Muller, Jerome Boateng
,Franck Ribery,Holger Bastuber, Robert Lewandowski na Mario Gotze.
Nayo
Paris St. Germain ya Ufaransa imesonga mbele hatua ya robo fainali
baada ya kuwaondoa Chelsea katika mashindano hayo japo timu hizo
zilitoka sare ya magoli mawili kwa miwili lakini magoli ya ugenini
iliyoyafunga hapo jana ndio yaliyowanufaisha Paris St. Germain.
Hivyo
mshindi katika mechi hiyo ilibidi kupatikana katika dakika thelathini
za nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika huku timu zote
zikiwa zimefungana goli moja kwa moja.
Wakiwa na matumaini ya
kuingia robo fainali Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli
kupitia Gary Cahill katika 81 lakini Mlinzi wa zamani wa Chelsea David
Luiz akafutilia ndoto hizo mbali baada ya kusawazisha goli hilo katika
dakika ya 86.
Na hivyo hadi dakika 90 za kwanza zinamalizika
Chelsea 1 na Paris St. Germain 1 na hivyo kulazimika kucheza dakika 30
nyingine ili kumpata mshindi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
CHELSEA WAONDOLEWA UEFA WAKIWAA KWAO...!!!
Vinara wa ligi kuu ya England,
Chelsea leo usiku wamejikuta wakiambulia majonzi baada ya kutolewa
katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya na Wapinzani PSG huku
wakiwa mbele ya mashabiki wao kunano Uwanja wa Stamford Bridge baada ya
kulazimishwa sare ya 2-2.
Licha ya PSG kucheza wakiwa
pungufu kwa kipindi kirefu kufatia Nyota wake Zlatan Ibrahimovic kupewa
kandi nyekundi ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi Oscar katika
dakika ya 32 kipindi cha kwanza, hawakuweza kuvunjika Moyo zaidi
waliongeza nguvu na kusaka ushindi hatimaye sasa Wametinga hatua ya Robo
fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya Vilabu.
Chelsea ndio walianza kupata bao
kupitia kwa Gary Cahill kunako dakika ya 80 kipindi cha pili kufatia
kona iliyopigwa na mabeki wa PSG wakashindwa kuosha mbele ndipo mchezaji
huyo akafumua shuti ambalo lilitinga kambani, Bila kukata tamaa
Wafaransa hao (PSG) walikomaa na kujipatia bao la kusawazisha katika
dakika ya 85 kupitia kwa David Luiz, ambapo hadi dakika 90 zinamalizika
Chelsea ilikuwa imebanwa mbavu na PSG kwa kukubali sare ya 1-1.
Kama kawaida ziliongezwa dakika
30 ili kupatikana mbabe wa mchezo, Thiago Silva beki wa PSG akanawa
mpira katika eneo la 18 na muamuzi akawazawadia Chelsea Penati ambayo
ilipigwa na Eden Hazard na kuipatia timu yake bao la 2 ikiwa ni dakia ya
95. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wednesday, March 11, 2015
TAZAMA PICHA ZAIDI ZA AJALI YA BASI LA MAJINJAH LILILOANGUKIWA NA KONTENA ENEO LA CHANGALAWE MAFINGA MKOANI IRINGA...!!!
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
HII NDIO ORODHA YA ABIRIA WALIOANZIA SAFARI STENDI KUU MBEYA, NANE NANE, UYOLE NA CHIMALA NA BASI LA MAJINJAH SPECIAL
Thursday, February 19, 2015
HAYA NDIO MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA, PAUL MAKONDA, SHABAN KISSU...!!!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi.
Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishiri na saba (27) zilizotokana na:
a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b)Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa wakuu wa Wakuu wa Mikoa:
c)Kupangiwa Majukumu Mengine wakuu wa Wilaya 7; na
d)Kutengua uteuzi wa Wakuu Wawilaya wengine 12.
katika babadiliko hayo Rais Kikwete amewateua wakuu wapya wa Wilaya 27 kujaza nafasi hizo zilizo achwa wazi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Aidha, Wakuu wa Wilaya siti na nne (64) wamebadilishwa vituo vyao vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa.
Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishiri na saba (27) zilizotokana na:
a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b)Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa wakuu wa Wakuu wa Mikoa:
c)Kupangiwa Majukumu Mengine wakuu wa Wilaya 7; na
d)Kutengua uteuzi wa Wakuu Wawilaya wengine 12.
katika babadiliko hayo Rais Kikwete amewateua wakuu wapya wa Wilaya 27 kujaza nafasi hizo zilizo achwa wazi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Aidha, Wakuu wa Wilaya siti na nne (64) wamebadilishwa vituo vyao vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa.
Walio teuliwa ni pamoja na Zelothe Steven (Musoma), Mboni
Muhita(Mufundi), Paul Makonda (Kinondoni), Shaabani Kissu (Kondoa)
Subscribe to:
Posts (Atom)