katika michuano ya Kombe la
Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, timu ya Simba imetinga hatua
ya nusu fainali baada ya kuichakaza Taifa Jang'ombe mabao 4-0 katika
mchezo wa robo fainali uliochezwa jana usiku mjini Zanzibar. Michezo
mingine ya robo fainali inaendelea leo kwa timu za KCC ya Uganda
kumenyana na Polisi Zanzibar, Azam ya Tanzania itakwaruzana na Mtibwa
Sugar pia ya Tanzania, huku Yanga ikikamilisha michezo ya hatua hiyo kwa
kupambana na JKU ya Zanzibar saa mbili usiku mjini Zanzibar. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Thursday, January 08, 2015
FERNANDO TORRES AREJEA KWA KISHINDO
Fernando
Torres arejesha ushindi katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa
kuwabamiza Real Madrid 2-0 katika michuano ya Kombe la Mfalme, Copa del
Rey.
Mbele ya umati wa mashabiki 46,800 waliokuwa wakiishuhudia
mechi hiyo ya aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu za Liverpool na Chelsea,
amerejea katika timu yake iliyomkuza na kumtambulisha kipaji chake,
Atletico Madrid.Raul Garcia,aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 58 akifunga kwa njia ya penalti, huku Jose Maria Gimenez akikamilisha ushindi wa Atletico kwa kufunga bao kwa njia ya kichwa katika dakika ya 76 ya mchezo.
Torres mwenye miaka 30 alibadilishwa katika dakika ya 59. Mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka katika timu ya Italia ya AC Milan wiki iliyopita, ndiye aliyeongoza kwa ufungaji katika timu ya Atletico kwa misimu mitano kabla hajatia mguu Liverpool mwaka 2007.
Mashabiki wapatao 45,000 waliishuhudia mechi iliyopigwa katika uwanja wa Vicente Calderon mnamo siku ya Jumapili wakati ambapo utambulisho wa Torres ulipofanyika na papo hapo jezi zenye jina lake zikaanza kuuzwa ambapo ndani ya saa 24, ziliuzwa jezi 2,000. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
STEVEN GERRARD AKARIBISHWA LA
Mchezaji
maarufu wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Brayant katika
kuonyesha umoja michezoni amemtumia ujumbe nahodha wa timu ya Liverpool
Steven Gerrard, baada ya uthibitisho kutoka timu ya LA Galaxy kwamba
kiungo huyo mkabaji ataungana na timu hiyo mwaka huu.
Katika
ujumbe wake wa video kwa Steven, Brayant anamwambia mchezaji huyo wa
zamani wa timu ya England kuwa yeye ni shabiki wake wa muda mrefu na kwa
hilo Brayant anaamini ushindi mwingine unakuja kwa timu ya Galaxy, na
anathibitisha ushindi upo, maana ana imani na Steven Gerrard.Gerrard atakipiga katika ligi kubwa za vilabu baada ya mkataba wake wa awali na Anfield kumalizika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wednesday, January 07, 2015
CCM, CUF WALIANZISHA
Utata mpya
umeibuka kuhusu matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya
wagombea watatu waliotangazwa washindi kuwekwa kando ikidaiwa kuwa
badala yake walioshindwa waliapishwa kuchukua nafasi zao, hali iliyozua
vurugu kubwa zilizotulizwa na polisi kwa mabomu ya machozi Ubungo jana.
Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CUF wanaodai
wagombea wa chama chao ndiyo walioshinda, waliibuka na kutanda nje ya
Hoteli ya Landmark kupinga kuapishwa kwa baadhi ya wenyeviti wa Serikali
za Mitaa wa CCM katika Wilaya ya Kinondoni, hatua iliyosababisha baadhi
ya wagombea na mashabiki kushushiwa kipigo hadi polisi walipoingilia
kati kwa kurusha mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya.
Vurugu hizo zilizodumu kuanzia saa tatu hadi saa
tano asubuhi, zililenga kuzuia wateule watatu wa mitaa ya Ukwamani,
Pakacha na King’ong’o kuapishwa kwa madai kuwa siyo walioshinda.
Kwa upande mwingine, aliyekuwa mgombea wa Mtaa wa
Msisiri, Juma Mbena alivamia eneo hilo akidai kuwa Gasper Chambembe
(CUF), ambaye alishinda katika mtaa huo hakustahili kuapishwa, kitendo
kilichosababisha ashushiwe kipigo na wafuasi wa CUF. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MAFUTA YAZIDI KUSHUKA BEI NCHINI
Bei ya mafuta ya
petroli, dizeli na ya taa nchini inazidi kushuka kutokana na kuporomoka
kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia tangu Juni mwaka jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati
na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa bei ya rejareja ya
petroli kuanzia leo imeshuka kwa Sh74, dizeli kwa Sh62 na mafuta ya taa
kwa Sh54.
Bei hizo zinashuka wakati kukiwa na mjadala mkali
kuwa bei zilizopo sasa hazisadifu hali halisi ya kuporomoka kwa mafuta
ghafi yanayouzwa kwa Dola 50 za Marekani kwa pipa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ZIARA YA MH. RIDHWANI KIKWETE JIMBONI KWAKE CHALINZE
Ridhiwani
akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara
ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuwashuru kwa
kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya
wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa
ardhi.
Mkazi
wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani
Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
Mkazi
wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x
zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo
alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo
kusababisha kukosa maendeleo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UTATA WAJITOKEZA KIFO CHA MESHACK YEBEI
hali
tata imezidi kujitokeza juu ya kifo cha Meshack Yebei, anayetajwa kuwa
shahidi katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Shahidi huyo alitarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC dhidi ya naibu Rais wa Kenya.Lakini mwishoni mwa wiki mwili wa Yebei ambao ulionekana kuunguzwa kiasi ,ulikutwa umetupwa kando ya mto huko Eldoret Magharibi mwa nchi hiyo.
Familia ya Yebei wanashuku kwamba chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni kumzuia ndugu yao asiweze kutoa ushahidi wake katika mahakama ya ICC huko The Hague. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SHELL YAKUBALI KULIPA FIDIA NIGERIA
Kampuni kubwa ya mafuta ya Shell imekubali kulipa dola milioni 80 kama fidia.
Kampuni hiyo ya Uholanzi imewapa fidia wakazi wa jamii ya Bodo katika eneo la Niger Delta walioathiriwa na uvujaji wa mafuta.Mawakili wa wavuvi 15,600 wa Nigeria wamesema wateja wao watapokea dola za Kimarekani 3,300 kila mmoja kutokana na hasara iliyosababishwa na uvujaji wa mafuta hayo.
"Kiasi kilichobaki cha dola milioni 30 zitatumika kwa ajili ya shughuli za jamii ya Bodo ambayo iliathirika vibaya kutokana na matukio mawili ya kuvuja mafuta mwaka 2008 na 2009".
Mawakili hao wamesema mafuta hayo yaliharibu maelfu ya hekta za mikoko kusini mwa Nigeria.
Fidia hiyo imesemekana kuwa kuwa kubwa kuwahi kuliko zote zilizowahi kulipwa nchini Nigeria, na hivyo kumaliza mvutano wa kisheria uliodumu kwa miaka mitatu. Wanaharakati wanasema kampuni ya Shell ililazimika kukiri kosa hilo mapema zaidi.
Matukio yote mawili ya kuvuja kwa mafuta yametokea katika bomba hilo hilo la Trans Niger Pipeline, linaloendeshwa na kampuni ya Shell, ambalo linachukua mafuta kutoka visima vyake(Shell) kwenda kituo cha mwisho cha kusafirisha mafuta hayo nje kilichopo pwani ya Bonny. Bomba hilo linasafirisha mapipa 180,000 ya mafuta kwa siku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KASEJA, YANGA GIZA NENE
IPO misemo mingi ambayo huashiria
kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao
dalili ya mvua ni mawingu.
Msemo huu unaweza ukawa na na
maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young
African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri
na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
jijini Dar es salaam.
Mchezaji huyo mwenye heshima
kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu
hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi,
lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji
wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili
ya ushiriki wa kombe la shirikisho.
Matukio hayo yote yameibua
maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya
mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na
mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga
kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..
Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.
Jerry Muro.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)