Maalim Hassan Hussein (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaama jana.
Maalim Hassan Hussein, ambaye ni
mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya
Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki
ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.
Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka
ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa
hospitali. Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: “Kiongozi huyo atakufa
wakati akipelekwa hospitalini.”
Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini
atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika
kutafuta sababu za kifo chake. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.