Wednesday, December 17, 2014

PLUIJM ATUA YANGA, MAXIMO ATIMULIWA MAZOEZINI

Kocha Hans van Pluijm akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam juzi, kuchukua mikoba ya Marcio Maximo aliyetupiwa virago Yanga. (Na Mpigapicha Wetu).

Kocha Hans van Pluijm akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimatafa wa Julius Nyerere Dar es Salaam juzi.

UONGOZI wa Klabu ya soka ya Yanga jana asubuhi ulilazimika kumwondoa mazoezini Kocha Mkuu, Marcio Maximo na kumrudisha klabuni ili kumalizana naye kabla ya kuanza safari ya kurudi kwao Brazil, huku akiiacha timu hiyo ikifundishwa na kocha anayetarajiwa kuchukua nafasi yake, Hans van Pluijm.

Maximo aliondolewa mazoezini na kupakiwa kwenye basi dogo la timu hiyo aina ya Toyota Hiace lililokuwa likiendeshwa na meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe.
Aliambana na msaidizi wake, Leonard Neiva na kiungo Emerson de Oliveira Roque aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea nchini Brazil.
Kitendo hicho kilitokana na uongozi huo kufikia makubaliano ya kumtimua kazi kocha huyo pamoja na msaidizi wake Neiva, kutokana na kushindwa kuipa mafanikio tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha miezi minne.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Kibarua chake kiliingia katika majaribu makubwa baada ya kufungwa mabao 2-0 na Simba katika pambano la Nani Mtani Jembe 2 mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam; matokeo yaliyosababisha afukuzwe.
Gazeti hili lilifika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola ambako Yanga wanafanyia mazoezi na kumkuta Maximo, Neiva na Emerson wakiwa ndani ya gari huku wengine wakiendelea na mazoezi na kumuuliza nini tatizo.
“Siwezi kuzungumzia chochote kwa sasa kwa sababu hata mimi sielewi tatizo ni nini, lakini ngoja tufike klabuni na baada ya mazungumzo na uongozi, nitajua cha kuzungumza na waandishi,” alisema Maximo akiwa ndani ya Hiace.
Baada ya gari hilo kuondoka Loyola, wachezaji wa Yanga waliendelea na mazoezi kama kawaida wakiwa chini ya kocha Pluijm aliyekuwa anasaidiana na makocha wazawa wakiwamo Juma Pondamali na Salvatory Edward.
Kwa upande wake, Pluijm aliyewasili nchini usiku wa kuamkia jana, alikataa kuzungumza kwa sababu hajasaini mkataba, lakini ana matumaini makubwa ya kufikia makubaliano baada ya kuzungumza na viongozi wa Yanga.
Taarifa ndani ya Yanga zinadai Maximo na wenzake wanatarajia kukutana na uongozi ili kumalizana kwa kulipwa haki zao ili waondoke huku Andrey Coutinho akiendelea kubaki kuitumikia timu hiyo kutokana na kuwa na mkataba mrefu.
Uongozi umedai Maximo alishindwa kuiongoza timu hiyo kumudu ushindani kwani licha ya kuwa nafasi nzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini imeshindwa kupata ushindi inapokutana na timu kubwa kama Simba na Mtibwa Sugar.
Maximo ameiongoza Yanga kushinda mechi tano za kimashindano kati ya nane ilizocheza timu hiyo inayoundwa na nyota wengi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na wengine kutoka Amerika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa ndani ya Yanga, Pluijm atapewa mikoba ya Jangwani akisaidiana na Charles Boniface Mkwasa ambaye kwa pamoja waliiongoza timu hiyo kwa takribani miezi mitano, kabla ya kuondoka wenyewe kwenda kufundisha soka ya kulipwa katika Klabu ya Al Shoalah ya Saudi Arabia.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Habari Leo

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...