Wednesday, December 17, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAMWAGA DAMU

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda. PICHA|MAKTABA 

Wakati tukio la Bukombe likihusisha mtu kuchinjwa katika sherehe za ushindi wa mkewe kuwa mwenyekiti wa mtaa, huko Nzega kijana moja alipigwa risasi na polisi wakati wa kusubiri matokeo ya uchaguzi huo.
Bukombe
Mume wa mshindi wa kiti cha mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kapela, wilayani Bukombe ameuawa baada ya kuchinjwa katika hafla ya ushindi wa mkewe.
Mtu huyo, Bundara James (56), aliuawa usiku wa kuamkia juzi katika Mtaa wa Kapela ulioko kwenye Kata ya Igulwa wilayani Bukombe muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kusherehekea ushindi huo.
Mke wa marehemu ambaye sasa ni mwenyekiti wa mtaa huo, Lusia Samwel alisema mumewe ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, alikutwa amechinjwa na watu wasiojulikana ambao walitoweka baada ya tukio hilo wakiacha panga walilofanyia uhalifu kwenye eneo la tukio.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Samwel aliibuka mshindi kupitia Chadema kwa kupata kura 463 akimwacha kwa mbali mpinzani wake kutoka CCM ambaye alipata kura 230.
Alisema baada ya ushindi huo, Chadema iliamua kufanya sherehe ya kumpongeza nyumbani kwake na ilipomalizika, mume huyo aliondoka nyumbani saa 1.13 jioni akiwa ameambatana na mwanaye wa kiume kurudisha vyombo vya muziki walivyokodi kwa ajili ya sherehe hiyo.
Alisema wakiwa wanakula chakula cha usiku ndani, mtoto alitoka nje na kurudi akikimbia: “Akasema mama kuna mtu amelala, tulipotoka nje tulikuta mume wangu amelala chini akiwa amechinjwa shingoni na panga limetelekezwa chini.” Alisema anaamini kuwa wauaji hao waliusogeza mwili wa marehemu karibu na nyumba yake.
Mtoto aliyemsindikiza baba yake kurudisha vyombo vya muziki, Rubeni Bundara alisema walifika salama na kukabidhi vyombo hivyo na baba yake akamwambia awahi nyumbani.
“Baadaye baba aliniambia mimi nirudi nyumbani nikapumzike. Sikujua kama angekutwa na umauti,” alisema.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...