Wednesday, December 17, 2014

MLIBERIA APATAITC, MUSHEED ASUBIRI SIMBA

Kpah Sherman

Kpah Sherman
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Kpah Sherman sasa ni ruksa kucheza katika Ligi Kuu baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuthibitisha kwamba hati yake ya uhamisho kumruhusu kucheza soka nchini tayari imeshafika.

Aidha, wakati Sherman akiwa na uhakika wa kuitumikia klabu hiyo, TFF imethibitisha kuchelewa kwa hati ya uhamisho ya kiungo mpya wa Yanga, Emerson de Oliviera Roque ambaye aliombewa ITC ili kuitumikia timu hiyo.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kukatwa kwa mchezaji huyo na nafasi yake kupewa aliyekuwa mchezaji wa Simba, Amisi Tambwe, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa ITC hiyo haijafika.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“ITC ya Emerson haijafika, lakini tayari maombi yalikwenda na kilichokuwa kinasubiriwa na majibu ya Shirikisho la Soka Brazil,” alisema Wambura.
Mchezaji mwingine ambaye hajapata ITC ni Juuko Musheed aliyesajiliwa Simba hivi karibuni ambaye pia maombi yake yanasubiriwa kutoka Victoria University ya Uganda.
Kwa mujibu wa Wambura, maombi ya ITC zao yalitakiwa kufika jana mchana na kwamba iwapo yatafanikiwa Yanga italazimika kukata mchezaji mmoja, ili wabaki watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Aliwataja wachezaji wengine waliopata ITC kuwa ni Abdul halim Humud aliyetoka Sofapaka kwenda Coastal Union, Brian Majwega aliyetoka KCC ya Uganda kwenda Azam FC, Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia kuja Simba, Simon Sserunkuma kutoka Victoria University aliyesajiliwa Simba na Paschal Wawa kutoka El Merreikh kwenda Azam FC.
Kuhusu wachezaji ambao wamekwenda kwa mkopo na waliosajiliwa, Wambura alisema itajulikana baadaye kwa vile maombi ya wachezaji hao hupitia mtandao na sio makaratasi tena.
Wambura alisema kwa mujibu wa Kanuni, wachezaji wasiozidi watano ndio ambao huruhusiwa kwenda kwa mkopo kutoka timu moja kwenda nyingine na hiyo ni kwa timu zote kuanzia Ligi Daraja la Kwanza. Alisema wiki ijayo Kamati ya Sheria ya TFF itakaa kuangalia timu zilizozingatia kanuni za uhamisho na ambazo hazijazingatia.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...