Wednesday, December 17, 2014

NAPE: KAKOSA YA CCM YAMEINUFAISHA UKAWA

 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. PICHA|MAKTABA 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kilifanya makosa katika baadhi ya maeneo ambayo yamekigharimu na kusababisha wananchi kupiga kura za hasira kukiadhibu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi huo ambao umeonyesha kuvinufaisha vyama vya upinzani kupitia umoja wao wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Nape alisisitiza kwamba makosa hayo ndiyo yaliyosababisha wapinzani kujinyakulia mitaa kadhaa kwa wepesi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.


“Tumejifunza na tumekuwa tunajaribu kila wakati kubadili mfumo wetu wa kura za maoni lakini bado kumekuwa na matatizo. Kwa mfano, kuna Mtaa Mwenge Dar es Salaam, wanaCCM waliamua kumchagua mgombea wa upinzani baada ya jina la waliyempenda kutorudi,” alisema Nnauye na kuongeza:

“Tunajua kwamba kuna maeneo mengi ambayo wapinzani wameshinda. Ukiangalia CCM tulifanya makosa katika kumweka mgombea, hivyo kusababisha hasira ambazo kwa kweli zimewafurahisha wapinzani lakini sisi zimetugharimu,” alisema.

Alisema chama chake kitafanya tathmini ili kubaini kama sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kupoteza baadhi ya mitaa.

Hata hivyo, Nape alisema wapinzani hawapaswi kuufurahia ushindi walioupata, bali iwe ni changamoto kwao katika kuhakikisha wanawatumikia wananchi waliowaamini.

Mwelekeo

Matokeo ya awali yameendelea kupatikana katika maeneo mbalimbali nchini yakionyesha kuimarika kwa upinzani na baadhi ya vyama kuongeza ushindi maradufu, licha ya kwamba CCM imeendelea kuwa na mitaa, vijiji na vitongoji vingi kuliko vyama vingine.

Wakati mwaka 2009 Chadema ilikuwa na jumla ya mitaa na vijiji 413 nchi nzima, matokeo ya awali yaliyolifikia gazeti hili hadi jana, kimeshajizolea viti 809.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, NCCR-Mageuzi kilichokuwa na mitaa/vijiji 39 mwaka 2009, hadi sasa kimeshajipatia 94 wakati CUF kilichokuwa na mitaa/vijiji 540 hadi sasa kina viti 285.

Chama kipya cha Alliance for Change (ACT - Tanzania) ambacho hakikuwapo mwaka 2009, kimejitutumua na hadi sasa kimeshapata mitaa/vijiji 10.
Wakati vyama hivyo vya upinzani vikionyesha kuimarika, isipokuwa CUF, CCM tayari imejinyakulia jumla ya mitaa na vijiji 2,882 ikilinganishwa na 12,042 vya mwaka 2009. Vyama vinavyounda Ukawa mwaka 2009 vilikuwa na jumla ya vijiji/mitaa 992 na sasa imeshajizolea 1,292.
Tathmini inaonyesha kuwa wakati CCM ikiendelea kuota mizizi katika mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Katavi na ile ya Kusini, upinzani hususan Chadema, umeimarika katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Dar es Salaam na kwenye miji ya baadhi ya mikoa.
Matokeo zaidi
Chadema wilayani Karatu kimeendelea kuitesa CCM baada ya kushinda vijiji 30, dhidi ya 27 vya chama hicho tawala. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
 
Wilayani Geita CCM imeshinda vijiji 99 kati ya 142 vilivyofanya uchaguzi, Chadema vijiji 32 na CUF 11.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ali Kidwaka alisema matokeo hayo yameonyesha tofauti na hamasa kubwa ikilinganishwa na mwaka 2009.
Wilayani Rungwe CCM imepata vijiji 83, Chadema 15; Ileje CCM vijiji 53, Chadema 15, TLP kijiji kimoja na CUF kimoja; Kyela CCM vijiji 70 na Chadema vijiji 10.
Busokelo: CCM vijiji 51 dhidi ya vinne vya Chadema na kimoja CUF. Katika Wilaya ya Mbozi, CCM vijiji 93, Chadema 13.
Katika Wilaya ya Mwanga, CCM imeshinda vijiji 66, Chadema 6; Same CCM vijiji 78 na Chadema 17. Katika Wilaya ya Siha kwa CCM imepata vijiji 52 na Chadema vinane na Hai CCM vijiji 38 na Chadema 25.
Katika Wilaya ya Moshi Vijijini CCM imepata vijiji 76, Chadema 46, NCCR 27 na TLP vinane wakati katika Wilaya ya Rombo, CCM ina vijiji 36, Chadema 22 na Moshi Mjini CCM 28 na Chadema 26.
Wilayani Nachingwea, CCM imeshinda vijiji 100 kati ya 124 vilivyofanya uchaguzi, Chadema imechukua 12 CUF 12.
Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Charles Linda amesema CCM kimepata ushindi kwenye vijiji 26, Chadema 15 na CUF kimoja. Mpanda Mjini CCM imepata mitaa 28 na Chadema 13.
Dodoma Mjini: CCM imenyakua vijiji vyote 19 na katika mitaa 170, chama hicho kimechukua 164 dhidi ya mitano ya Chadema.
Kondoa CCM imepata vijiji 71, CUF 19 na Chadema kimoja wakati Wilaya ya Chemba CCM imeshinda katika vijiji 73, Chadema tisa na CUF 14. Wilayani Kongwa, vijiji vyote 87 vimechukuliwa na CCM.
Katika Wilaya ya Mpwapwa, CCM imechukua vijiji 102 kati ya 113 vilivyofanya uchaguzi na Chadema imeambulia kimoja na Bahi CCM imechukua vijiji 53 kati ya 59 vilivyofanya uchaguzi, Chadema vinne na TLP kimoja.
Ikungi, Chadema vijiji 49, CCM 41 na CUF vinne.
CCM imenyakua vijiji 357 kati ya 523 vilivyofanya uchaguzi, CUF 148 na Chadema vitatu.
Katika Wilaya ya Ukerewe, Chadema imepata vijiji 47, CCM 27 na CUF vijiji viwili
Imeandikwa na Lauden Mwambona, Stephano Simbeye, Christopher Lilai, Kibada Ernesst, Josephine Sanga, Mussa Juma, Shakila Nyerere, Mwanja Ibadi, Jovither Kaijage, Daniel Mjema na Beatrice Moses na Gasper Andrew.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year. 

Na Mwananchi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...