Wednesday, March 06, 2013

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN MJINI MAGHARIBI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein, akionesha zawadi aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis,(katikati) alipofika Ofisini kwake akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza leo,(kushoto) Mkuu wa Wilaya Mjini, Abdi Mahmoud Mzee.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme, Hassan Ali Mbarouk,(kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo.
 Msoma Utenzi, Shadat Juma,akiwaburudisha wananchi katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha Mafunzo ya Kazi za Amali,Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi,  mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika ziara Mkoa huo.
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya Ujenzi kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Iddi Khatib,alipotembelea kukagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini Zanzibar,akiwa katika ziara ya mkoa Mjini Magharibui iliyoanza leo. 

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme, Hassan Ali Mbarouk,(wa pili kushoto) wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...