Kampuni ya simu ya mkononi ya safaricom yashutumiwa Uchaguzi Kenya Nairobi,Kenya
KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Safaricom inatuhumiwa kula njama ya kumuingiza madarakari mgombea wa Jubilee Uhuru Kenyatta,Safaricom inadaiwa kuchakachua
matokeo hayo kabla ya kuyarusha kwenda tume ya Uchaguzi. Kwa muujibu wa taarifa
zilizolifikia Habarimpya.com
hivi punde inadai kwamba tume ya Uchaguzi nchini humo imekesha
usiku kucha kujadili suala hilo huku ikitafuta namna ya kuzuia machafuko
yanayohofiwa kutoka nchini humo.
"SIRI KUBWA YAFICHUKA KUHUSU
UCHAKACHUAJI WA MATOKEO YA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2013 NCHINI KENYA
NA KUSABABISHA MIKUTANO KIBAO KUTAFUTA KUOKOA HALI
KUSITOKEE MACHAFUKO"kilisema chanzo hicho. Siri kubwa yabainika nchini
Kenya muda si
mrefu kuhusu utitiri wamatokeo
kutoka mashinani na jinsi gani yalivyokua yakichakachuliwa na Injinia
wa kampuni ya Simu Safaricom kabla ya kukabidhi matokeo hayo kwa tume ya
uchaguzi na vyombo vya habari nchini humo. Safaricom ni kampuni ya simu
iliojitolea kusaidia
tume ya uchaguzi
kutoka mashinani na kutarajiwa kuzikabidhi kwa wahusika bila ya
kuvurugwa kwa namna yoyote ile lakini uhalisia wa mambo haukua hivo.Hali
hiyo ilionekana
kumkera sana meneja mkuu wa
kampuni hiyo ya simu mara baada ya kubaini kwamba hadi hivi sasa sehemu
kubwa ya matokeo yanayorushwa hewani kamwena yale yaliopokelewa
na kampuni yake tangu awali kiasi cha kumfanya kuchapisha katika rundo
la makaratasi 'matokeo halisi' anayodai kuwa ni tofauti kabisa na
yale yanayoendelea kuzungushwa kote katika vyombo vya habari
nchini humo. Kwa msingi wa hali hiyo ya sintofahamu katika
uchaguzi wa Kenya kuna madai kwamba kuna misururu ya mikutano inayoendelea hadi hivi
sasa nyuma ya pazia kutafuta namna gani ya kudhibiti taarifa hizi zisiwafikie wananchi wa
nchi hiyo kwa ujumla wao na pengine kusababisha hasira na michafuko.source jamii foram
No comments:
Post a Comment