Wednesday, March 06, 2013

Rais Hugo Chavezi wa Venezuela afariki dunia baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.


Rais Hugo Chavez enzi za uhai wake.
Rais Hugo Chavez wa Venezuela amefariki dunia baada ya kuugua kwa miaka miwili ugonjwa wa saratani na hivyo kufikisha ukingoni uongozi wake wa miaka kumi na nne katika taifa hilo la Amerika ya kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ametangaza kupitia kituo cha televisheni ya nchi hiyo kuwa Chavez mwenye umri wa miaka 58 ameaga dunia na kusema kifo chake kimewaacha na uchungu mwingi.
Chavez amefariki katika hospitali ya kijeshi huko Caracass baada ya kuugua kwa muda na kufanyiwa upasuaji mara nne uliosababisha afya yake kuzorota.
Serikali ya Venezuela imetangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa na kwamba Rais huyo atazikwa Ijumaa wiki hii.
Mwezi Oktoba mwaka jana Chavez alishinda uchaguzi lakini hali yake ya afya haikuwa nzuri hivyo kushindikana kumuapisha.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...