SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF)
limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha
kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13
alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na
hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani
hapo
Akizungumza kwa niaba ya viongozi
wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na
moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia
kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko
kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo..
.
Alisema kuwa wasanii wanatakiwa
kujifunza kutoka kwake kwani wanahitaji kuwa kitu kimoja kujaliana
kwenye matatizo na kutambua kuwa wao ni familia moja wanaojenga nyumba
moja
"Kitendo alichoonyesha msanii
mwenzetu ni kitendo cha kuigwa na cha kiimani siyo kwamba anauwezo sana
hapana ila kujali na utu ndio kilichomsukuma atoe fedha hizo" alisema
Mwakifwamba
"Unajua kuwa nacho na kutoa ni
vitu tofauti wengi pale walikuwa navyo ila labada hawakuwa na moyo wa
kutoa hivyo Wema mungu atambariki na kumuongezea pale alipopunguza "
aliongeza Mwakifamba
Mwakifamba alimtaka Kajala kutoa
shukurani kwa mungu kwa kumsaidia kumtoa kule alipokuwa kwani sehemu
yenye mateso na inayoumiza katika maisha ya kila siku
Wakati huo huo kwa upande wake Msanii
Wema Sepetu "Imenichukua masaa mawili kufanikisha hili,nilienda benki
nikatoa fedha na kuja hapa kulipa, ni sh.milioni 13".Hii ni kauli ya
Msanii wa Filamu Wema Sepetu akizungumza na waandishi wa habari buda
mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kumlipia faini ya kiasi hicho cha
fedha msanii mwenzake Kajala Masanja.
Wema alisema kuwa mumlipia
Kajala kiasi hicho cha fedha haoni kama amepoteza kwani msanii huyo ni
kama ndugu yake wa karibu.
"Katika vitu vingi
sana,kumsaidia kwangu sijaona kama nimepoteza chochote,naona kama
nimetoa kitu kama mtu yoyote anayeweza kufanya hivi kwasababu kutoa ni
moyo,sihitaji kulipwa chochote mwenyezimungu ndiye atanilipia"alisema
Aliongeza kuwa "Nahakika hakuna
mtu anayependa kukaa gerezani,kwahiyo nimeona kama nitafanya hivyo
nitamuokoa katika hali zote mbaya"
Kwaupande wake Dkt.Cheni
alimewataka wasanii nchini kuwa na ushirikiano pale mmoja wao anapopatwa
na matatizo kwani wao ni kitu kimoja na ni familia moja hivyo
kushirikiana kwao ndio kutaendelea kuimalisha undugu walio nao na
kufanikiwa katika kazi wanayoikusudia
Alisema katika maisha hakuna
mtu aliyewekwa alama usoni kuwa atakuwa wa matatizi tu bali kila mtu
anaweza kupata tatizo kwa aina yoyote hivyo tunatakiwa tuwe karibu.
"Kiukweli sina la kusema zaidi
kwani matatizo yanamkuta kila mtu na yanapokukuta unakuwa haujajua,Mtu
unaweza kuona unafanya jambo sahihihi lakini kijamii au kisheria
linakuwa tatizo,ninachoomba kwa wasanii wenzangu tuwe na ushirikiano
pale mwenzetu anapopatwa na tatizo kama hili tujitoe kwa
mwenzetu"Alisema Dkt.Cheni.
Awali Dk.Cheni alisema kuwa
wangeweza kuchangishana kiasi hicho cha fedha na kuzilipa lakini baadaye
Wema alionekana akitoka mbio katika viwanja vya mahakama hiyo na kwenda
katika gari lake ambapo ilidaiwa alikwenda benki kutoa fedha.
Kajala alitoka gerezani baada
ya kulipiwa kiasi hicho cha fedha na msanii mwenzake Wema Sepetu muda
mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment