Sunday, September 28, 2014

YANGA ‘WAKITAITIWA’ SAFU YA KIUNGO..JAJA ATAISHIA KUZUNGUKA TU!

Jaja akipambana

Jaja alishindwa kufunga dhidi ya Mtibwa na kwa bahati mbaya alikosa mkwaju wa penalti
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
YANGA SC wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara, septemba 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar, leo jioni wanaikaribisha Tanzania Prisons katika mtanange wa raundi ya pili uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Prisons wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting waliopata katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa wikiendi ya septemba 20 mwaka huu uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, September 27, 2014

UKAWA WASEMA JK, CCM HAWAELEWEKI



 
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema kuwa Rais Jakaya Kikwete na CCM hawaeleweki ukidai ni kutokana na kukiuka makubaliano yao kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

Umoja huo pia umedai kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kutoa uamuzi fasaha kuhusu tafsiri ya kisheria ya mamlaka ya Bunge hilo katika kurekebisha Rasimu ya Katiba kwa kuogopa lawama kutoka Ukawa na CCM.

Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP, NLD na NCCR-Mageuzi ulieleza hayo jijini hapa jana ulipozungumzia Mchakato wa Katiba ulipofikia, hasa baada ya Bunge hilo kufanya marekebisho ya kanuni kwa wajumbe wake kuruhusiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa kwa Bunge hilo kati yao na Rais Kikwete yameshindwa kutekelezwa, jambo ambalo wanashindwa kuelewa sababu zake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAJI WARIOBA AWAPANIA WAJUMBE WA KATIBA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dar es Salaam jana.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba imeondoa mambo manne muhimu yaliyokuwa kiini cha kupata Katiba ya mageuzi.
Akiyataja mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma,  madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,” aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 19 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema rasimu hiyo inatofautiana kwa kiasi kikubwa na rasimu iliyotolewa na tume hiyo Desemba mwaka jana.
“Sina hakika kama tutapata Katiba Mpya labda Katiba iliyoboreshwa. Rasimu au Katiba itakayopendekezwa na Bunge Maalumu haitapigiwa kura hadi 2016. Sina hakika kama kura hiyo itapigwa kwa kuwa hakuna maridhiano hasa kuhusu muungano,  rasimu hiyo itaanza kupingwa tangu siku ya kutolewa kwake,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 27, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KESI YA MUBARAK YAAHIRISHWA MISRI

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa mahakani
Uamuzi wa kesi inayomkabili rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kuhusu mashtaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 umeahirishwa.
Jaji alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sahabu ya kuwepo kwa ushahidi ambao bado mahakama haijausikiliza.
Wakati wa kesi ya leo kanda moja ya video ilionyesha mrundiko wa stakabadhi za ushahidi.
Bwana Mubarak alipatikana na hatia mnamo mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini baadaye hukumu hiyo ikabatilishwa.
Mahakama hiyo imesema kuwa itatoa hukumu yake mwezi Novemba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...